| Swahili
AFRIKA
1 dk kusoma
Taasisi ya kupambana na rushwa Nigeria yafungia akaunti za serikali ya jimbo
Hatua hii imezidisha msuguano kati ya taasisi hiyo ya serikali kuu na ile ya Jimbo la Osun, ambayo imeshtumu EFCC kwa kufanya kazi nje ya misingi ya kisheria
Taasisi ya kupambana na rushwa Nigeria yafungia akaunti za serikali ya jimbo
Gavana Adeleke anasema kufungwa kwa akaunti kutatatiza shughuli za serikali wakati wa kipindi cha uchaguzi.

Tume ya kupambana na rushwa nchini Nigeria (EFCC), imeagiza kufungwa kwa akaunti za Serikali ya Jimbo la Osun la Kusini Magharibi mwa nchi hiyo, ikieleza wasiwasi wake kuhusu fedha za umma zinazohusishwa na uchunguzi unaoendelea wa madai ubadhirifu wa fedha karibu Naira bilioni 11 ($8,080,000).

Katika taarifa ilioweka kwenye mtandao rasmi wa X, EFCC ilisema uchunguzi ulianza Machi 2026 na unaangazia madai ya matumizi mabaya ya fedha kutoka serikali ya taifa.

Hatua hii imezidisha msuguano kati ya taasisi hiyo ya serikali kuu na ile ya Jimbo la Osun, ambayo imeshtumu EFCC kwa kufanya kazi nje ya misingi ya kisheria na jaribio la kuingilia masuala ya jimbo hilo kabla ya uchaguzi wa ugavana.

Tume hiyo inasema maafia kadhaa, ikiwemo Mhasibu Mkuu wa jimbo, tayari wameshahojiwa kama sehemu ya uchunguzi.

Osun inapinga hatua hiyo

Serikali ya Jimbo la Osun inapinga vikali hatua hiyo, ikiieleza kuwa kinyume na sheria na yenye njama za kisiasa.

Gavana Adeleke anaeleza kuwa kufunga akaunti kutakwamisha shughuli za serikali wakati wa kipindi cha uchaguzi na kudai kuwa hatua hiyo inalenga kudumaza serikali yake kabla ya uchaguzi wa ugavana.

CHANZO:TRT Afrika Swahili