Namna mradi wa dola milioni $240 unavyotoa fursa kwa jamii za pwani ya Benin na Mauritania

Mradi huo wa Benki ya Dunia unalenga kuwalinda watu wa maeneo ya pwani ya Benin na Mauritania dhidi ya mmonyoko wa udongo na mafuriko huku ukiimarisha uchumi unaotokana na bahari.

By Pauline Odhiambo
Benki ya Dunia imeidhinisha dola milioni $240 kwa lengo la kusaidia miradi ya pwani za Benin na Mauritania. / Wengine

Itakapofika hatua ya bahari kuharibu shamba la mihogo la baba yake, Bernard Koffi, ambaye ni mvuvi katika kijiji cha Hillacondji, Benin, tayari anakuwa ameshajifunza kuhusu mabadiliko ya mienendo ya bahari. Kwa miaka kadhaa, chanzo cha Mto Mono — unaotumika kusafirisha bidhaa za kilimo na usafiri wa watu — kimekuwa kikibadilika, kuwa kipana zaidi na hatari.

“Maji yalikuwa hayatupi tabu,” Bernard anaiambia TRT Afrika akiwa amesimama katika sehemu ambayo wakati mmoja ilikuwa mita mia mbili kutoka ufukweni. “Sasa hivi, yanakuja majumbani mwetu. Tunapoteza sehemu zetu kila msimu wa mvua.”

Wiki kadhaa zilizopita, Bernard alipata taarifa ambazo zilibadilisha mtazamo wake kutoka kukata tamaa hadi kuwa na matumaini. Benki Kuu ya Dunia imeidhinisha dola milioni 240 kwa lengo la kusaidia kubadilisha muonekano wa pwani hiyo.

“Wanasema wataimarisha fukwe zetu na kurudisha mikoko,” anasema, akionesha ardhi oevu. “Kama mikoko itarudi, samaki watakuwa na sehemu ya kujifika na kuzaliana. Kwa sisi, hiyo siyo kujali mazingira tu; hiyo ni fedha kwetu.”

Kukabiliana na mafuriko

Mradi huo, unaojulikana kama Mradi wa Uchumi wa Bahari wa Afrika Magharibi (WACA+), umekuja wakati muafaka. Maeneo ya pwani ya Afrika Magharibi ni miongoni mwa maeneo yenye uwezo mkubwa kiuchumi, ilhali miongo kadhaa ya mmonyoko wa udongo,mafuriko, na mazingira mabaya — yaliyosababishwa na mabadiliko ya tabianchi — yamesababisha hasara ya mabilioni kwa uchumi.

Kwa mataifa kama Benin na Mauritania, ambapo wanategemea zaidi miundombinu ya pwani, utalii, na uvuvi, hatari iko wazi. Mpango huo mpya unalenga kulinda watu zaidi ya nusu milioni kutokana na mmonyoko wa udongo na mafuriko huku wakitengeneza ajira za karibu watu 13,000 kwa awamu ya kwanza.

Nchini Mauritania, hatari iko nje kidogo ya mji mkuu. Katika mitaa ya pwani ya Nouakchott, wakazi wanaishi katika hofu ya dhoruba. Kwa Fatimetou Mint El Arbi, muuza samaki na mama wa watoto wanne, dhoruba hizo hutatiza biashara yake.

‘Uchumi unaotokana na bahari’

Chini ya mradi huo wa Benki Kuu ya Dunia, Mauritania itapata fedha ya kuimarisha mifumo ya kuzuia dhoruba. Lakini kwa Fatimetou, mabadiliko makubwa ya mradi huo siyo tu kwa muonekano wake — bali ni kwa uchumi pia.

Mafunzo na kulinda mazingira

Mbali za miundombinu, mradi huo unalenga kurudisha hadi heka 3,000 za mikoko na ardhi oevu ya pwani —kinga asili ya mafuriko ambayo pia inatoa fursa kwa samaki kuzaliana. Wakati huo huo, utatoa msaada wa kitaalamu, mafunzo, na fedha kwa ajili ya sekta ndogo ndogo kuanzia uvuvi na utalii.

Kufikia 2031, watu zaidi ya 31,000 wanatarajiwa kufaidika na mradi wa mafunzo na umarishaji wa biashara, huku awamu zingine baadaye zikitarajiwa kusaidia upatikanaji wa ajira zaidi ya 50,000.