Uturuki imesema kuwa mashambulizi ya hivi karibuni ya Israel dhidi ya Gaza yamethibitisha tena kwamba serikali ya Waziri Mkuu, Benjamin Netanyahu, haina nia ya kuleta amani na Wapalestina.
"Lengo pekee la Netanyahu ni kuwahamisha Wapalestina kutoka katika ardhi yao ya asili na kuzuia kuwepo kwa amani na utulivu katika eneo hilo," Wizara ya Mambo ya Nje ilisema katika taarifa.
Taarifa hhiyo Ilisema Netanyahu anaendelea kuchukua hatua zinazodhoofisha usawa wa kikanda na juhudi za upatanishi zinazoongozwa na nchi, haswa Marekani.
"Imekuwa muhimu kwa jumuiya ya kimataifa kuchukua msimamo thabiti zaidi na imara dhidi ya mbinu ya Netanyahu ya kujitanua," taarifa hiyo iliongeza, ikitoa wito kwa washirika wa kimataifa kuzingatia maadili ya kibinadamu.
Majeruhi wa raia
Mashambulizi ya Israel kote Gaza katika siku mbili zilizopita yameua raia na kuharibu vifaa muhimu vya matibabu, mjumbe mkuu wa Bodi ya Amani, Nickolay Mladenov, alisema Jumapili.
"Mashambulizi ya siku mbili kote Gaza yameua raia na kuharibu vifaa vya matibabu ambavyo watu wanategemea," Mladenov aliandika kwenye X.
Mladenov alisema ongezeko hilo lilikuja baada ya "juhudi kubwa" za Bodi ya Amani na wapatanishi kutoka Uturuki, Misri, Qatar na Marekani ili kupata makubaliano ya Palestina kwa ramani ya utekelezaji kamili wa mpango wa Gaza wa Rais wa Marekani Donald Trump.
Mashambulizi ya Israel yaliwaua Wapalestina wasiopungua 19, wakiwemo watoto watatu na mtoto mchanga, na kuwajeruhi wengine kadhaa siku ya Jumapili, katika ukiukaji wa hivi karibuni wa mpango wa kusitisha mapigano ulioanza kutumika tangu tarehe 10 Oktoba 2025.
Mashambulizi hayo yalitokea siku moja baada ya Wapalestina wanane kuuawa na wengine kujeruhiwa Jumamosi.






















