| Swahili
AFRIKA
1 dk kusoma
Rais Samia Suluhu Hassan kuzindua Hospitali ya Mwalimu Nyerere nchini Angola
Kiongozi huyo wa Tanzania, anatarajiwa kuzindua hospitali ya rufaa iliyopewa jina la Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, iliyopo jijini Luanda Angola.
Rais Samia Suluhu Hassan kuzindua Hospitali ya Mwalimu Nyerere nchini Angola
Rais Samia Suluhu Hassan wa Tanzania.

Rais Samia Suluhu Hassan wa Tanzania anatarajiwa kuzindua hospitali ya rufaa iliyopewa jina la Mwalimu Julius Kambarage Nyerere jijini Luanda, anapoanza ziara yake ya kikazi nchini Angola, Julai 31, 2026.

Kulingana na taarifa iliyotolewa na Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais ya  Tanzania, Rais Samia anatarajia kushiriki hafla ya uzinduzi huo, akiwa na mwenyeji wake Joao Manuel Goncalves Lourenco.

Hafla hiyo ya uzinduzi, pia itahudhuriwa na Mama Maria Nyerere, mjane wa Mwalimu Nyerere.

Wakati huo huo, Rais Samia atafanya mazungumzo na mwenyeji wake pamoja na kushiriki hafla ya chakula cha jioni iliyoandaliwa na Wake wa Marais wa Afrika, kwa lengo la kuchangisha fedha za utekelezaji wa shughuli za kijamii na kiuchumi za uwezeshaji wa wanawake na vijana.

Ziara hiyo ni mwendelezo wa kuimarisha uhusiano wa kihistoria na wa kindugu kati ya Tanzania na Angola, uliojengwa tangu enzi za harakati za ukombozi wa Bara la Afrika, kulingana na taarifa hiyo.

CHANZO:TRT Afrika Swahili
Soma zaidi
Edward Kijanangoma atawazwa mfalme mpya wa Tooro
Je, Afrika itapata viti vya kudumu katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa?
Jeshi la Polisi Tanzania laonya wanaochochea mgomo wa madereva wa mabasi
Madaktari bingwa wa Tanzania waweka kambi ya matibabu Malawi
Makamu wa Rais Tanzania ataka vijana kupewa fursa za mafunzo ya ajira
Jeshi la Sudan lapinga madai ya kuunga mkono makundi ya upinzani Ethiopia
Uchaguzi Mkuu kurejesha utulivu Sudan Kusini?
Marekani italazimika kuondoka Mashariki ya Kati: Iran
Mashambulizi ya kigaidi mjini Mogadishu yapungua kwa karibu asilimia 90: Serikali ya Somalia
Maambukizi ya Ebola nchini DRC ni zaidi ya 8,000 tangu kuanza kwa mlipuko huo
Watoto 17 miongoni mwa wahamiaji 250 waliookolewa katika pwani ya Mauritania
Marekani kusitisha ufadhili wa sekta ya afya nchini Zimbabwe kufikia mwishoni mwa mwezi wa Septemba
Mwanamke wa kumi apatikana amefariki katika msururu  wa mauaji nchini Afrika Kusini
Qatar Airways yakopesha marubani kwa shirika la ndege la taifa la Rwanda
Wapiganaji wa RSF wahamia upande wa jeshi la Sudan baada ya kushuhudia 'maafa'
Mkuu wa Umoja wa Mataifa asikitishwa kwa kunyimwa viza  kiongozi wa Sudan, Burhan kuhudhuria UNGA
Jenerali wa DR Congo miongoni mwa watu 13 waliofariki katika ajali ya ndege
Afrika itapata hadhi ya uwanachama wa kudumu katika Baraza la Usalama Umoja wa Mataifa?
Sudan yashtumu taarifa za Marekani zinazohoji uhalali wa serikali huku viza ya Burhan ikizua utata
Mke wa Besigye awataka viongozi wa Afrika wazungumzie masuala ya haki za binadamu