Wanajeshi wa Nigeria waua zaidi ya magaidi 20 kaskazini mashariki mwa nchi, jeshi linasema
Wanajeshi wa Nigeria wamewaua magaidi wasiopungua 20 katika jimbo la kaskazini mashariki mwa nchi la Yobe, jeshi limesema siku ya Alhamisi.
Wanajeshi wa Nigeria wamewaua magaidi wasiopungua 20 katika jimbo la kaskazini mashariki mwa nchi la Yobe, jeshi limesema siku ya Alhamisi.
Haya yanajiri baada ya mashambulio ya magaidi siku ya Jumatatu kuua watu wasiopungua 14, ikiwemo wanajeshi 10 katika majimbo ya Borno na Yobe, kulingana na vyanzo vya kiraia na kijeshi vya eneo hilo.
Msemaji wa jeshi katika kanda Sani Uba amesema katika taarifa ilotolewa siku ya Jumatano kuwa wamefanikiwa kutibua "mashambulizi" yaliyofanywa na magaidi hao kwa kambi ya jeshi ya Goniri, jimbo la Yobe, usiku wa kuamkia Jumanne.
"Magaidi zaidi ya 20 walikatwa makali, ikiwemo kamanda mwandamizi wa magaidi hao aliyejulikana kwa jina la Abu Yusu, Munzir wa Dursula," Uba alisema.
Nigeria yaongeza juhudi dhidi ya ugaidi
Uba amesema kuwa baadhi ya wanajeshi walijeruhiwa, bila kusema idadi yao.
Mkazi wa kijiji cha karibu cha Katarko aliiambia AFP maoema wiki hii kuwa magaidi waliwaua wanajeshi wanne na kuchoma moto majengo na magari ya kijeshi Goniri.
Ugaidi katika kanda umesababisha vifo vya watu zaidi 40,000 na kuacha karibu milioni mbili bila makazi, kulingana na Umoja wa Mataifa.
WIki iliopita, wanajeshi saba na raia 11 waliuawa wakati magaidi wa Boko Haram walipovamia kambi moja na kushambulia miji ya karibu ya Ngoshe wiliaya ya Gwoza, karibu na mpaka wa Cameroon, kufyatua risasi na kuwateka wengine nyara.
Nigeria imeongeza juhudi katika vita vyake dhidi ya ugaidi, huku tishio likiwa zaidi kutoka kwa Boko Haram.