Serikali ya Burundi imetangaza mlipuko mwingine wa ugonjwa kipindupindu nchini humo.
Akizungumza na waandishi wa habari, Waziri wa Afya wa nchi hiyo, Lydwine Baradahana alisema ya jitihada za kuudhibiti ugonjwa huo, bado hali si ya kuridishisha kwani kuna jumla ya wagonjwa 34 wanaopokea matibabu.
“Hii ni mara ya kwanza kwa mwaka kukutana na hali kama hii,” alisema waziri huyo.
Kulingana na Barahadana, wagonjwa wapya walikuwa wakipokea matibabu katika vituo mbalimbali vya afya, ikiwemo hospitali ya Prince Regent Charles.
Alitadhaharisha kuhusu uchafu wa mazingira, akisema kuwa ndiyo sababu kubwa iliyopelekea maambukizi hayo mapya.
Serikali ya Burundi ilitenga Dola milioni 1 katika robo ya kwanza ya mwaka 2026, kwa ajili ya kupambana na ugonjwa huo.
Kulingana na Shirika la Kuhudumia Watoto la Umoja wa Mataifa (UNICEF), mataifa 23 yalikumbwa na ugonjwa wa kipindupindu mwaka jana.
















