Iran imesema meli sita zimejaribu kupita katika njia ambayo hairuhusiwi katika Mlango Bahari wa Hormuz mapema Jumatatu baada ya kuzima mifumo yao ya usafiri wa majini, kwa mujibu wa shirika la habari la serikali la IRIB.
Meli hizo zimejaribu kuvuka katika njia ya kimkakati ya kusini ambayo ni "hatari na kinyume cha sheria," chanzo cha uhakika kimeiambia IRIB.
Chanzo hicho kimedai kuwa meli hizo vilikuwa zinajaribu "kuchokoza" vikosi vya Marekani vilivyopo eneo hilo.
Meli moja ilihusika moja kwa moja, huku nyengine zikielekezwa upande wa Ghuba chini ya udhibiti wa Iran, kwa mujibu wa ripoti.
Hakuna taarifa zaidi iliyotolewa kuhusu meli hizo, bendera zake, wafanyakazi au aina ya tukio.
Chanzo kimesema njia hiyo ya meli kupitia Mlango Bahari wa Hormuz imeelezwa wazi kuwa ni hatari na haipitiki.
Jeshi la Marekani halikutoa taarifa yoyote mara moja.
Hali ya wasiwasi kati ya Marekani na Iran imeongezeka katika wiki za hivi karibuni, huku Marekani ikiishambulia Iran, wakati huo huo Iran ikijibu kwa kushambulia maeneo ya Marekani yaliyopo katika eneo hilo, ikiwemo Bahrain, Jordan and Kuwait.
Julai 8, Rais wa Marekani Donald Trump alitangaza kusitishwa kwa makubaliano ya amani na Iran, huku akiilaumu kwa kukiuka makubaliano hayo.
Marekani imetaka Mlango Bahari wa Hormuz kutumika bila kizuizi, huku Iran ikisisitiza kuwa meli sharti zipite katika eneo ambalo linadhibitiwa na mifumo yake.
Trump ameamrisha Jeshi la Marekani kutoanzisha mashambulizi mapya dhidi ya Iran, baada ya wiki mbili za mashambulizi ya kila siku, imeripoti Axios Jumamosi, kwa kunukuu vyanzo vinavyofuatilia uamuzi huo.
















