Kifo cha Saif Al-Islam Gaddafi na athari zake kwa siasa za Libya
Kifo cha Saif Al-Islam Gaddafi kinaashiria kufungwa kwa kitabu cha nafasi ya familia ya Gaddafi katika siasa za Libya.
Muda mfupi baada ya kuuawa kwa Saif Al-Islam Gaddafi, macho na masikio ya wengi yameelekezwa kwenye hatma ya kisiasa ya nchi hiyo.
Yawezekana, huo ndio ukawa mwisho wa enzi wa familia ya Gaddafi, kwenye siasa za Libya.
Saif Al-Islam alikuwa mtoto wa pekee katika familia ya Gaddafi aliyekuwa na haina ya kisiasa.
Na ndiye aliyedhaniwa kuwa mrithi wa Gaddafi, baada ya kuwa ameandaliwa kuchukua uongozi kutoka kwa baba yake.
Muktadha mzima wa mauaji yake bado unaibua mjadala.
Hata hivyo, licha mabadiliko ya kisiasa yanayoendelea, jambo moja linabakia kuwa wazi: Enzi za familia ya Gaddafi zimefikia kikomo kufuatia kifo cha Saif Al-Islam.
Hamu ya mageuzi ya mwaka 2011
Historia fupi ya kisiasa ya Saif Al-Islam, inaweza kutufungulia macho kuhusu mwisho wake wa kusikitisha.
Ilianzia katikati ya miaka 2000, wakati Saif Al-Islam alipojijengea umaarufu mkubwa ndani ya siasa za Libya.
Ni katika kipindi hichi, alipojulikana zaidi kwa fikra zake za kimageuzi.
Baadhi ya mifano ya hamu yake ya mabadiliko na mageuzi, ni pamoja na mikakati mbalimbali, ikiwemo “Libya Al-Ghad”, yaani Libya ya Kesho.
Mradi huu ulionesha matumaini makubwa, hasa katika kukuza haki za kibinadamu.
Mkakati huu, uliwezesha kuanzishwa kwa taasisi ya Benghazi, ambayo ilihusisha familia za waathirika wa tukio la mauaji ya Abu Salim ya mwaka 1996.
Mageuzi hayo hayo, yaliwezeshwa kuachiwa huru kwa wafungwa wa kisiasa, wakiwemo wale waliohusishwa na vikundi vya kidini.
Hata hivyo, mikakati hiyo tajwa hapo, ilipelekea kuanguka kwa utawala uliokuwa madarakani, kufuatia maandamanio ya Busleem ya Februari 2011, ambayo yaliamsha mapinduzi ya Libya.
Cha kushangaza ni kuwa, mapinduzi hayo, yalimpa Saif Al-Islam fursa adimu ya kudhihirisha uadilifu wake, anapoingia kwenye safari ya kisiasa.
Iwapo mpango wake wa kisiasa ungeenda vizuri, basi angechagiza mageuzi na maridhiano kwa wakati huo.
Badala yake, aliwakejeli wapinzani hadharani, ambao walikuwa ni wawakilishi wa watu wa Libya, akiwaambia “kunyweni maji ya bahari”, iwapo hawakuridhishwa na utawala uliokuwa madarakani.
Hii, ilitoa tafsiri kuwa mpango wake kisiasa, ulikuwa gheresha tu.
Ujio wake wa pili kisiasa
Ilipofika mwaka 2017, Al-Islam aliachiwa kutoka gereza alilokuwa akishikiliwa toka mwaka 2011.
Hapo ndipo alipoanza kuonesha hamu ya kurudi kwenye ulingo wa siasa, akiainisha, hali mbaya ya Libya.
Hata hivyo, licha ya kutaka kuwepo na maridhiano, bado hakuwa tayari kujiweka kando na kauli za kale za Libya, ambazo ziliwakera Walibya wenyewe.
Badala yake, alijihusisha na vitendo vilivyotia dosari uchaguzi wa mwaka 2021.
Safari fupi ya Al-Islam kisiasa inaakisi makosa yake na kuanguka kwa urithi wa kisiasa, hali iliyoathiri mustakabali mzima wa hali ya kisiasa nchini Libya.
Yahya Habil, ni mwandishi wa habari wa kujitegemea kutoka Libya, aliyejikita kwenye masuala ya Afrika.