| Swahili
AFRIKA
1 dk kusoma
Shabiki maarufu ‘Lumumba Vea’ akosa viza ya kwenda kuishangilia DRC dhidi ya Jamaica
DRC itakuwa ikisaka nafasi ya kushiriki michuano ya Kombe la Dunia kwa mara ya pili, baada ya kushiriki mwaka 1974, wakati huo ikijulikana kama Zaire.
Shabiki maarufu ‘Lumumba Vea’ akosa viza ya  kwenda kuishangilia DRC dhidi ya Jamaica
Shabiki soka maarufu wa DRC, Lumumba Vea./Picha:Wengine
tokea masaa 6

Michel Kuka Mboladinga, yule shabiki, aliyepata umaarufu mkubwa wakati wa fainali za AFCON 2025 nchini Morocco, atakosa kushiriki mechi ya kufuzu fainali za Kombe la Dunia, baada ya kukosa viza ya kusafiri hadi Mexico.

DRC itakutana na Jamaica, Aprili 1, 2026 katika mechi ya kufuzu michuano hiyo mikubwa, inayoandaliwa kwa pamoja na Marekani, Canada na Mexico.

Hatua hiyo, itamlazimu ‘Lumumba Vea’ kubakia nchini DRC, akiishangilia timu ya taifa ya nchi hiyo, maarufu kama The Leopards.

“Iwe mbali au karibu, tutaendelea kuishangilia Leopards,” alisema Lumumba.

Hata hivyo, ‘Lumumba Vea’, bado ana nafasi ya kupata Visa nyingine kwa ajili ya michuano ya Kombe la Dunia iwapo DRC itafuzu , zikiwa zimebaki siku 72, kabla ya kuanza kwake.

Mboladinga, maarufu kama Lumumba Vea, alijozoelea umaarufu kutokana na mtindo wake wa kusimama wima muda wa michuano hiyo, akimuiga Waziri Mkuu wa zamani wa DRC, Patrice Lumumba.

DRC itakuwa ikisaka nafasi ya kushiriki michuano ya Kombe la Dunia kwa mara ya pili, baada ya kushiriki mwaka 1974, wakati huo ikijulikana kama Zaire.

CHANZO:TRT Afrika Swahili