| Swahili
AFRIKA
1 dk kusoma
Shirika la Afya Duniani (WHO) lathibitisha maambukizi ya kirusi cha Hanta
Shirika la WHO lilisema siku ya Jumanne, kuwa linaendelea kufanya mawasiliano na mgonjwa mmojawapo aliyesafiri na meli hiyo Aprili 25, 2026, kati ya Saint Helena na Johannesburg.
Shirika la Afya Duniani (WHO) lathibitisha maambukizi ya kirusi cha Hanta
Ugonjwa huo uliripotiwa wakati wa safari meli kutoka Ushuaia nchini Argentina kuelekea Cape Verde./Picha:Wengine

Shirika la Afya Duniani (WHO) limethibitisha maambukizi mawili ya virusi vya Hanta kati ya watu waliokuwa ndani ya meli ya kitalii huko Cape Verde.

Kulingana na WHO, watu wengine watatu wamepoteza maisha kutokana na ugonjwa huo.

Shirika la WHO lilisema siku ya Jumanne, kuwa linaendelea kufanya mawasiliano na mgonjwa mmojawapo aliyesafiri na meli hiyo Aprili 25, 2026, kati ya Saint Helena na Johannesburg.

"Kufikia Mei 4 mwaka huu, maambukizi mapya ya ugonjwa huo yameripotiwa, ikiwemo vifo vya watu watatu, mmoja akiwa na hali mbaya kwa sasa,” lilisema shirika hilo.

Ugonjwa huo uliripotiwa wakati wa safari meli kutoka Ushuaia nchini Argentina kuelekea Cape Verde.

CHANZO:AFP