| Swahili
AFRIKA
1 dk kusoma
Maelfu watoroka Akobo, Mashariki mwa Sudan Kusini
Maelfu ya raia wamekimbia ngome hii ya upinzani huku jeshi likisema utekelezaji wa agizo hilo ni muhimu ili kusafisha njia ya mashambulizi ya kijeshi.
Maelfu watoroka Akobo, Mashariki mwa Sudan Kusini
Mji wa Akobo upo karibu na mpaka wa Ethiopia. / TRT Afrika Swahili
tokea masaa 10

Umoja wa Mataifa umeonesha wasiwasi kuhusu uwezekano wa kuongezeka kwa hali ya mbaya ya kibinadamu nchini Sudan Kusini.

Hii inafuatia agizo la Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Sudan Kusini (SSPDF) Machi 6, 2026 la kuwataka raia, kikosi cha Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini, mashirika ya Umoja wa Mataifa na mashirika yasiyo ya kiserikali kuondoka katika kaunti ya Akobo iliyopo mashariki mwa nchi.

Mji wa Akobo upo karibu na mpaka wa Ethiopia.

Maelfu ya raia wamekimbia ngome hii ya upinzani huku jeshi likisema utekelezaji wa agizo hilo ni muhimu ili kusafisha njia ya mashambulizi ya kijeshi.

Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Uratibu wa Masuala ya Kibinadamu inasema Mji wa Akobo ambao kwa sasa unahifadhi takriban watu 270,000, wakiwemo waliokimbia makazi yao awali ambao wanategemea usaidizi wa kibinadamu kwa ajili ya kuishi.

Umoja wa Mataifa unasema hatua zozote za kijeshi ndani au karibu na eneo hilo lenye idadi kubwa ya watu zitawaweka raia kwenye hatari kubwa ya kusababisha janga la kibinadamu katika Kaunti ya Akobo.