Somalia yashtumu uteuzi wa balozi wa Israel katika eneo lililojitenga la Somaliland
Somalia imetaja hatua hiyo ya Israel kama iliokiuka uhuru wake, na umoja, ikitoa wito kwa mashirika ya kimataifa kuzingatia sheria ya kimataifa, kwa kuwa hilo ni wazi linakwenda kinyume na taratibu za Umoja wa Mataifa, pamoja na Umoja wa Afrika
Siku ya Alhamisi Somalia ilishtumu vikali uteuzi wa balozi wa Israel kwa sehemu iliojitenga ya Somaliland, ikiutaja kuwa ukiukwaji uhuru wake na ukiukwaji wa wazi wa sheria ya kimataifa, na kusisitiza kuwa eneo hilo linabaki kuwa sehemu ya nchi yao.
“Hatua hii ni wazi kuwa imekiuka uhuru na umoja wa Somalia. Hili linakwenda kinyume cha sheria ya kimataifa, ikiwemo utaratibu wa Umoja wa Mataifa na misingi ya Umoja wa Afrika, wote ambao wanatambua Somalia kama taifa moja, na uhuru ndani ya mipaka inayotambulika ya kimataifa,” Wizara ya Mambo ya Nje ilisema katika taarifa.
Inasema Somalia inakataa kabisa jaribio lolote la kutambua kidiplomasia au kisiasa sehemu yoyote ya eneo laeke nje ya mamlaka ya serikali kuu ya Somalia.
“Mpango wowote unaolenga kutenganisha hauna msingi wa kisheria na unadumaza makubaliano ya kimataifa yaliyowekwa,” taarifa hiyo ilisema.
Inasema nchi itaendelea kufanya kazi kwa karibu na washirika wa kimataifa ili kuimarisha taarifa za umma, utawala wa kidemokrasia, maridhiano ya kitaifa, na kukabiliana na ugaidi.
Somalia inasema hatua ya Israel inahatarisha kuzua taharuki katika kanda.
Somalia pia ilitoa wito kwa Israel kutafakari na kubadilisha uamuzi wake na kuheshimu kikamilifu uhuru wa mipaka, na wa kisiasa wa Somalia, akitoa wito kwa mashirika ya kimataifa kusimamia sheria ya kimataifa na “kukataa hatua zozote ambazo zitakiuka umoja wa Somalia au kuhalalisha madai ya kujitenga."
Israel amemteua Michael Lotem kama balozi wake wa kwanza kwa eneo hilo lililojitenga la Somaliland siku ya Jumatano.
Disemba 2025, Israel ilitangaza kutambua Somaliland, hatua iliopingwa vikali na serikali ya Somalia na kushtumiwa na nchi nyingi kote duniani.