“Leo, miezi miwili baada ya kusambazwa kwa majeshi kwa kiwango kikubwa zaidi na uchokozi uliofanywa na wanyanyasaji katika eneo hili, pamoja na kushindwa kwa fedheha kwa Marekani katika mipango yake, sura mpya inaanza kujitokeza katika Ghuba ya Uajemi na Mlango wa Hormuz,” alisema Kiongozi Mkuu wa Iran Mojtaba Khamenei katika ujumbe uliosomwa kupitia televisheni ya serikali.
Marekani yatathmini kutumia makombora ya kasi ya juu dhidi ya Iran
Kamandi Kuu ya Marekani imeomba kupelekwa kwa mfumo wa makombora ya kasi kubwa zaidi unaojulikana kama Dark Eagle katika Mashariki ya Kati ikionesha “uwezekano wa kutumika dhidi ya Iran,” kulingana na ripoti ya Bloomberg iliyonukuu vyanzo mbalimbali.
Iwapo ombi hilo litaidhinishwa, itakuwa mara ya kwanza kwa Marekani kupeleka mfumo huo, ambao bado haujatangazwa rasmi kuwa uko tayari kwa matumizi kamili ya kijeshi.
Ripoti hiyo ilieleza kuwa ombi hilo lilichochewa na hatua ya Iran kuhamisha vifaa vyake vya kurushia makombora kwenda maeneo yaliyo nje ya masafa ya kombora la mashambulizi ya (Precision Strike Missile), silaha yenye uwezo wa kulenga na kushambulia shabaha kwa usahihi wa hali ya juu katika umbali unaozidi maili 300 (takribani kilomita 483).










