21 wauwawa katika shambulio la waasi mashariki mwa DRC
Katika tukio hilo, wanamgambo walishambulia vijiji vitatu vya Boti, Isigo na Mambimbi vilivyo Kaskazini mwa Kivu na kuharibu mali pamoja na kuua watu.
Watu wapatao 21 wamepoteza maisha kufuatia shambulizi lililofanywa na waasi wa kikundi cha ADF, mashariki mwa DRC.
Tukio hilo lilitokea siku ya Ijumaa katika kitongoji cha Lubero.
“Idadi ya vifo katika shambulio imefikia 21 toka ile ya awali ya 14,” alisema kiongozi wa kikundi cha Bapakombe, Boniface Kanyamulamba, katika mahojiano yake na wanahabari.
“Vijiji vitatu, kikiwemo cha Boti, Isigo na Mambimbi vilishambuliwa katika tukio hilo.”
Mashambulizi hayo yamesababisha watu wengi kupoteza makazi yao, huku wengine wakizikimbia nyumba zao, na kuelekea mji wa Kambau.
Hali ya usalama katika eneo hilo, limeathiri shughuli za kila siku, ikiwemo elimu, biashara na nyinginezo.
Mwaka 2025, taifa la DRC, lilikumbana na changamoto ya kibinadamu, kufuatia milipuko ya magonjwa, migogoro ya kivita na mabadiliko ya tabia nchi.