| Swahili
AFRIKA
2 dk kusoma
Jeshi la Nigeria lakanusha kuhusu mashambulizi yake kuua raia, lasema majambazi 70 wameuawa
Makao Makuu ya Jeshi yanasema operesheni dhidi ya makundi yenye silaha katika eneo hilo itaendelea wakati maafisa wa usalama wakikabiliana na majambazi na kurudisha hali ya usalama.
Jeshi la Nigeria lakanusha kuhusu mashambulizi yake kuua raia, lasema majambazi 70 wameuawa
PICHA YA MAKTABA: Jeshi la Nigeria limetetea mashambulizi yake angani likisema ni muhimu dhidi ya makundi hayo yenye silaha. / Reuters

Jeshi la Nigeria limekanusha taarifa zinazodai kuwa raia waliuawa wakati wa mashambulizi ya angani katika eneo la Shiroro, Jimbo la Niger, likisisitiza kuwa operesheni hiyo ililenga majambazi na kusababisha vifo vya wapiganaji kadhaa.

Katika taarifa siku ya Jumapili, Mkurugenzi wa Jeshi wa Masuala ya Habari, Meja Jenerali Michael Onoja, alisema mashambulizi yalianzishwa baada ya taarifa za kijasusi kuonesha kuwa majambazi walikuwa wamekusanyika katika Kijiji cha Lukupe eneo la Shiroro Mei 9, 2026.

Kulingana na Makao Makuu ya Jeshi, droni za jeshi la Nigeria zilifanya mashambulizi ya angani kati ya saa tano na dakika hamsini na tisa usiku Mei 10 na saa kumi na mbili asubuhi, zikilenga maficho ya majambazi maeneo ya vijiji vya Katerma, Bokko, Kusasu na Kuduru.

Onoja anasema taarifa za kijasusi zilizopatikana kutoka kwa vyanzo vya maeneo hayo zinaonesha kuwa mashambulizi hayo “yalikuwa mahsusi” katika vijiji vya Kusasu, Katerma na Bokko, kukanusha madai kuwa raia waliuawa.

Kukabiliana na ukosefu wa usalama

Alieleza kuwa majambazi karibu 70 wameuawa katika kijiji cha Kusasu pekee, huku wapiganaji walionusurika wakionekana kuondoa miili ya wenzao kwa ajili ya kwenda kuzika.

“Kwa mujibu wa majukumu ya Jeshi la Nigeria la kufanya operesheni ya kumaliza ukosefu wa usalama kote nchini, taarifa za kijasusi zilionesha majambazi wamekusanyika katika kijiji cha Lukupe huko Shiroro,” taarifa hiyo ilisema.

“Wakati huo huo, Kitengo cha Jeshi la Nigeria cha droni, kufuatia taarifa za kijasusi, kilifanya mashambulizi kadhaa ya angani katika maeneo mbalimbali ya makundi hayo, ikiwemo vijiji vya Katerma, Bokko, Kusasu na Kuduru. Taarifa zaidi kutoka kwa vyanzo vya eneo hilo zimethibitisha kuwa mashambulizi hayo yalilenga maeneo mahsusi yaliyokusudiwa.”

Mashambulizi ya angani ya jeshi la Nigeria dhidi ya makundi yenye silaha yametegemea zaidi droni katika maeneo ya vijijini ambapo makundi hayo yenye silaha yako kwenye misitu na sehemu zisizofikika kwa urahisi. Hata hivyo, mashambulizi ya angani ya siku zilizopita yamezua utata kufuatia matukio ya raia kuuawa kimakosa katika mashambulizi hayo.

CHANZO:TRT Afrika English
Soma zaidi
Shirika la Fedha Afrika kumpa Dangote milioni $600 kwa ajili ya miradi ya mbolea Nigeria, Ethiopia
Siasa za lawama: Kwa nini wahamiaji wamekuwa walengwa katika mzozo wa kiuchumi wa Afrika Kusini
Chama cha upinzani Nigeria chafungiwa kushiriki katika uchaguzi wa 2027
Watu 28 wafariki nchini Ethiopia baada ya basi kutumbukia kwenye korongo
Shirika la Madaktari Wasio na Mipaka MSF yawafuta kazi wafanyakazi 18 kwa kuwadhulumu wakimbizi
AU,Misri yaridhishwa na makubaliano ya amani Marekani na Iran
Maambukizi ya Ebola nchini DRC yamepanda hadi 710 huku idadi ya waliofariki ikifikia 149
Polisi wakamata nge 150 katika uwanja wa ndege wa Afrika Kusini
Nigeria imewaua 'wapiganaji wa kigaidi' 13,000  katika mwaka uliopita: Rais Tinubu
Ndege ya kurudisha wahamiaji wa Marekani yatua  Jamhuri ya Afrika ya Kati
Kuanzia 'kuishi hadi mafanikio: Kwa Nini mjadala kuhusu ulemavu wa ngozi unabadilika
Wataalamu wa Kiafrika wanyimwa viza za Umoja wa Ulaya kwa mkutano mkuu wa wakunga
Kombe la Dunia: Mchezaji wa Ghana Thomas Partey azuiwa kuingia Canada
Mashambulizi ya Ukraine yanaathiri uchumi wa Urusi, lakini pia “unaimarika kwa haraka”: Putin
Mauritania yawaokoa wahamiaji 500 ndani ya siku 10 huku wengi zaidi wakijaribu kuvuka
Misri yatoa wito kwa Marekani, Iran 'kwa fursa' ya makubaliano baada ya Trump kusitisha mashambulizi
Ronaldo na Messi Kombe la Dunia mara ya 6
"Makubaliano makubwa" yamefikiwa na Iran: Trump
Bajeti ya trilioni 62.33 Tanzania na kupanda kwa gharama ya maisha
Raia 262 wa Nigeria wanaokimbia mashambulizi dhidi ya wageni Afrika Kusini warudishwa nyumbani