Nigeria imesema siku ya Ijumaa kuwa inapanga kuwasafirisha raia wake zaidi ya 1,000 kutoka Afrika Kusini huku vurugu dhidi ya wahamiaji zikiongezeka nchini humo, ambapo kwa muda mrefu imekuwa pendwa kwa wafanyakazi wa Afrika waliokuwa rasmi na wale ambao si rasmi.
Hatua hii ya Nigeria inakuja baada ya hivi majuzi Ghana kuwarudisha nyumbani mamia ya raia wake kutoka Afrika Kusini katika kukabiliana na machafuko yanayolenga raia wa kigeni.
Ukaguzi wa raia wa Nigeria wanaotaka kuondoka kwa hiari ulianza siku ya Alhamisi, msemaji wa wizara ya mambo ya nje Kimiebi Ebienfa aliiambia AFP siku ya Ijumaa.
"Idadi kamili bado haijatolewa," alisema. "Tunatarajia watu zaidi ya 1,000."
Katika taarifa iliyotolewa siku ya Jumanne, Balozi wa Nigeria nchini Afrika Kusini anasema "imejadili na nchi wenyeji kuhusu kufutiwa makosa kwa watu" ili wale walio "na makosa yanayohusiana na uhamiaji" waruhusiwe kuondoka na kurudi nyumbani kuliko kuzuiliwa.
Changamoto za ajira
Hadi hivi karibuni,Afrika Kusini, nchi iliokuwa zaidi kiviwanda barani Afrika, imekuwa ikipata wafanyakazi kutoka kote barani.
Lakini kuelemewa na idadi kubwa ya ukosefu wa ajira zaidi ya asilimia 30, imefanya kuwa na maandamano ya chuki -- ikiwemo vurugu za wiki kadhaa zilizopita.
Vurugu za hivi karibuni zimeibua mijadala kote Afrika kuhusu chuki, uhamiaji, na tofauti kati ya maneno matupu juu ya Uanamajumui na uhalisia unaokabili uhamiaji katika bara.
Muda wa mwisho uliotangazwa na kundi la wazawa wanaopinga uhamiaji haramu wa Juni 30 umezua hofu baada ya maandamano dhidi ya wahamiaji wiki kadhaa zilizopita kusababisha vifo vya watu kadhaa.
























