Tanzania dhidi ya Morocco kutafuta nafasi ya robo fainali
Siku ya Jumapili Tanzania inaingia dimbani tena kukabiliana na wenyeji wa AFCON 2025 katika harakati za kutafuta kufuzu robo fainali.
Taifa Stars ilimaliza ya tatu kwenye kundi C ikiwa na alama mbli pekee, na kufanikiwa kuingia hatua ya 16 bora ya mashindano hayo ya Afrika.
Taifa hilo la Afrika Mashariki lilipata sare katika mechi yake ya mwisho. Walikabiliana vikali na timu ambayo ni moja ya iliopewa nafasi ya ushindi Tunisia, waliomaliza katika nafasi ya pili na alama nne.
Timu ya taifa ya Morocco ilijikatia tiketi yake ya hatua hiyo ya 16 baada ya kumaliza kundi A ikiwa na alama saba. Walitoka sare ya 1-1 dhidi ya Mali, wakawafunga Visiwa vya Comoro na Zambia.
Mafanikio ya Simba hao wa Milima ya Atlas yamewapa hamasa mashabiki wa Morocco, wakiendelea kuamini kuwa timu yao ina nafasi kubwa ya kuchukua ubingwa.
Kocha Mkuu wa Morocco Walid Regragui amekiri kuwa timu inahitaji kujipanga vizuri ili kuwa na muendelezo wa matokeo chanya.
Iwapo vijana wa Miguel Gamondi, Tanzania watafanikiwa kuvuka hatua hiyo hadi robo, wataweka wanaweka historia nyingine kwa timu za Afrika Mashariki.