Je, Tanzania kuweka historia dhidi ya Tunisia AFCON?

Tanzania na Tunisia wanakabiliana kutafuta nafasi ya pili ya kufuzu moja kwa moja kutoka katika kundi C wakati watakapokutana uwanja wa Olimpiki mjini Rabat siku ya Jumanne.

By
Tanzania kuvaana na Tunisia. / CAFonline.com

Vijana wa Taifa Stars wanaingia uwanjani baada ya kupata sare ya 1-1 na jirani zao Uganda, huku wapinzani wao wakitafuta kuzinduka baada ya kufungwa 3-2 na Nigeria.

Tanzania ilianza mechi zake za AFCON vibaya, wakipoteza 2-1 kwa Nigeria, lakini haikushangaza kutokana na uwezo wa wapinzani wao hao wa Afrika magharibi.

Kushindwa huko kunamaanisha kama walitakiwa kuwa na matumaini ya kuingia hatua nyingine ya 16 bora kwa mara ya kwanza katika historia, ilibidi wapambane vikali dhidi ya Uganda.

Sasa, Taifa Stars wamerudi tena kutafuta kufuzu moja kwa moja kwenye kundi, na baada ya kutoka sare ya 1-1 na Cranes, wako nafasi ya tatu wakiwa na alama moja baada ya mechi mbili.

Matokeo hayo yanamaanisha ni fursa yao kujitetea ili waweke historia, na ushindi dhidi ya Tunisia siku ya Jumanne utawapata nafasi hiyo kuingia kwenye hatua ya 16 kwa mara ya kwanza kwenye mashindano hayo.