Kwa nini kuzuiwa kwa bandari kunazua taharuki Afrika Mashariki
Nchi ambazo hazina bandari kama Ethiopia na Uganda zinaongeza juhudi za kufikia bandari huku suala la uchumi likipewa kipaumbele na subira ya kidiplomasia ikififia.
Mataifa ya Mashariki mwa Afrika yanapigania kupata nafasi ya kutumia bandari, huku wakieleza kuchoshwa kwao na urasimu katika mipaka pamoja na gharama kubwa za uchukuzi.
Rais Yoweri Museveni wa Uganda alifikia hadi kutoa onyo kwa nchi jirani ya Kenya kabla ya baadaye kutuliza uhasama mwezi uliopita. Pamoja na kuwa ni kwa muda, sera hiyo ya hatari ilidhihirisha hali ya taharuki ya muda mrefu kwa Uganda kutumia njia ya Bahari Hindi.
"Bahari yangu ni Bahari Hindi," alieleza waandishi wa habari, akilinganisha hali hiyo na sehemu ya nyumba ambazo wakazi wa ghorofa za juu wana haki sawa na wale wanaoishi sehemu ya chini.
Upande wa kaskazini, kuimarika kwa maendeleo ya Ethiopia, ikiwa ni pamoja na mradi mkubwa wa bwawa na umeme barani Afrika na uwanja wa ndege mkubwa zaidi barani, kunatatizwa na kutoweza kufikia bahari.
Njia yake kuu ya kuingiza ni bidhaa ni kupitia Bahari ya Shamu katika nchi jirani ya Djibouti, ambao wanatoza mamilioni ya dola kwa mwaka kama kodi ya kutumia bandari, kulingana na maafisa.
Makampuni ya Ethiopia yanalipia dola bilioni moja zaidi kila mwaka kwa ajili ya ada ya usafirishaji wa mizigo.
Ikiwa na idadi ya watu milioni 100, Ethiopia ndiyo nchi ambayo haina bandari na yenye idadi kubwa zaidi ya watu duniani. Waziri Mkuu Abiy Ahmed ameweka wazimu nia yake ya kupata kufikia Bahari ya Shamu, ambayo Ethiopia ilipoteza wakati walipotengana na Eritrea 1993. Serikali yake inasisitiza kuwa inataka kutumia bandari hiyo kwa amani.
Wataalamu wanalaumu kuongezeka kwa uhasama kwa matumizi ya bandari kutokana na kufeli kwa dilplomasia na changamoto katika Jumuiya za kikanda.
"Kilichoandikwa na kinachofanyika ni vitu viwili tofauti. Inapokuja suala la utekelezaji, au sehemu ya utekelezaji au maslahi binafsi yanajitokeza. Hili ni suala ambalo linaathiri nchi nyingi ambazo hazina bandari katika kanda," Profesa David Mugisha, Mwanazuoni wa masuala ya uhusiano wa kimataifa, ameiambia TRT Afrika.
Jaribio la Ethiopia Januari 2024 kutaka kukodi kilomita 20 ya mwambao wa pwani kutoka kwa eneo lililojitenga la Somaliland lilizua taharuki ya kidiplomasia, huku Somalia ikishtumu Ethiopia kwa kudharau uhuru wa mpaka wake.
Juhudi za Uturuki za kuleta upatanishi ziliweka msingi wa kuleta amani kati ya mataifa hayo mawili jirani, kuelekea kupatikana kwa kile kilichojulikana kama Azimio la Ankara ambapo Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed na Rais Hassan Sheikh Mohamud wa Somalia walikubaliana kuheshimu uhuru wa mataifa yao.
Hata hivyo, Abiy anaendelea kuonesha nia ya kuwa na bandari ya bahari. Aliwaambia wabunge wa Ethiopia mwezi Oktoba kuwa "ana uhakika asilimia milioni moja" Ethiopia haitobaki kuwa nchi isiyo na bandari daima, "iwe mtu anataka au hataki".