| Swahili
MICHEZO
2 dk kusoma
Mkuu wa Shirikisho la UEFA hataki nafasi ya Infantino, anachotaka ni ajiuzulu
Ceferin anasema mpango wa Kombe la Dunia wa Infantino ‘ni mbovu kuliko wa Super League.’
Mkuu wa Shirikisho la UEFA hataki nafasi ya Infantino, anachotaka ni ajiuzulu
PICHA YA MAKTABA: Gianni Infantino (kushoto) na Aleksander Ceferin (kulia) walifanya kazi pamoja UEFA / Reuters

Rais wa Shirikisho la Soka barani Ulaya (UEFA) Aleksander Ceferin anasema hana nia ya kugombea nafasi ya Rais wa FIFA Gianni Infantino lakini anaonya kuwa Infantino atakabiliwa na upinzani iwapo atataka kugombea tena kwenye uchaguzi wa mwezi Machi.

Infantino amekabiliwa na shinikizo baada ya kuachana na mpango wake wa kuuza hisa za Kombe la Dunia kwa wawekezaji binafsi. UEFA na mashirikisho mengine walipinga mapendekezo hayo, huku UEFA ikitishia kususia mashindano ya FIFA.

Ceferin alishtumu mpango huo katika mahojiano ya kipindi cha podcast ‘The Rest is Politics’, akiutaja kuwa “mbovu kuliko mpango wa Super League.”

“Nina uhakika kuwa mpango huo [FFE] haupo tena. Kwangu mimi, jambo muhimu ni kwamba tumezuia jaribio lingine la kutaka kuweka rehani mchezo.” alisema.

Ceferin alisema Infantino sasa anaweza kuchagua kati ya mawili: aondoke madarakani baada ya kupoteza kuungwa mkono na wadau wa soka au agombee kwenye uchaguzi na kukabiliana na mpinzani.

“Moja ni atambue kuwa haungwi tena mkono, na siyo tu kutoungwa mkono na wale wanaopiga kura pekee, lakini kutoungwa mkono kabisa na wadau wa soka, mashabiki, wachezaji, wachezaji wa zamani, makocha.

“Ya pili ni kuwa ashiriki uchaguzi mwezi Machi, lakini kwa hali hiyo, nadhani kutakuwa na mgombea dhidi yake. Sijajua atakuwa nani.”

Infantino ameiongoza FIFA tangu 2016 na ameonekana kama atashinda bila kupingwa katika uchaguzi wa mwaka ujao nchini Morocco. FIFA imeweka Novemba 18 kama siku ya mwisho ya kuwasilisha majina ya wagombea.

‘Sina nia’

Ceferin, 58, ambaye ametajwa kama mmoja ya wagombea wa nafasi ya Rais wa FIFA, anasema yeye bado amejikita kwenye UEFA.

“Sina nia ya kugombea kwa sababu mbili. Sababu ya kwanza naipenda UEFA na napenda kufanya kazi hapa, na nadhani wakati fulani … ni wakati wa kufurahia maisha.

“Na la pili ni kuwa, sifa yangu itakuwa juu, juu zaidi iwapo sitogombea.”

Alipoulizwa kama Infantino amekuwa karibu sana na Rais Donald Trump, zaidi kabla ya mashindano ya Kombe la Dunia, Ceferin alisema: “Kwa kweli, utakuwa limbukeni kudhani kuwa mwanasiasa kama huyo, au mwanasiasa yoyote, ni rafiki wa dhati. Kipindi unakuwa na tatizo, unakuwa si rafiki tena wa mwanasiasa.”

CHANZO:Anadolu Agency
Soma zaidi
Guye na Tigst waongoza Ethiopia kufagia mbio za Berlin Marathon
Mo Salah hatacheza mechi ya kufuzu AFCON dhidi ya Sudan Kusini kutokana na nyasi bandia za Uwanjani
Mechi za kuwania kufuzu AFCON 2027 zinaanza huku kukiwa na utata kuhusu bingwa mtetezi
Agnes Ng’etich aweka rekodi mpya ya dunia katika mbio za nusu marathoni za wanawake pekee
Mkuu wa shirikisho la Afrika aunga mkono Tanzania, Kenya na Uganda kuandaa AFCON 2027
Kenya kuwa mwenyeji wa Mashindano ya Riadha ya Dunia 2029 ikiwa ya kwanza barani Afrika
FIFA yakanusha madai ya Morocco ya 'uwenyeji' wa mechi ya fainali ya Kombe la Dunia 2030
Erdogan akutana na timu ya Voliboli ya wanawake ya Uturuki baada ya ubingwa wa Ulaya
Timu ya wasichana ya Tanzania ya chini ya umri wa miaka 15 imetwaa ubingwa wa CECAFA
Mshambuliaji Aubameyang astaafu kuichezea timu yake ya taifa ya Gabon
Antonio Rüdiger astaafu kuichezea timu yake ya taifa
Jepchirchir anaongoza ushindi wa 1-2 kwa Kenya jijini Sydney
Gobena avunja rekodi ya Sydney Marathon huku Ethiopia ikitawala mbio za wanaume
Fenerbahce yaifunga Lyon 2-1 kuiwezesha kurejea Ligi ya Mabingwa Ulaya baada ya misimu 17
Bondia wa zamani bingwa wa dunia Zolani Tete auawa kwa kupigwa risasi nchini Afrika Kusini
Guinea yatangaza nia ya kuandaa Kombe la Mataifa ya Afrika
FIFA yawaadhibu wachezaji wa Argentina, yaitoza faini shirikisho kwa matukio ya Kombe la Dunia
Cristiano Ronaldo atangaza azma yake ya kustaafu soka
Algeria imefanikiwa kupata medali kwa mara ya kwanza katika mashindano ya WAFCON baada ya kuishinda
Afrika Magharibi ving’ang'anizi kwa mara ya kwanza kwa nafasi ya tatu WAFCON