| Swahili
ULIMWENGU
2 dk kusoma
Muungano unaoongozwa na Saudia watoa onyo huku wakiandaa oparesheni dhidi ya Houthi mjini Sanaa
Msemaji wa muungano huo anasema raia wametakiwa kuondoka ili waweze kufanya "mashambulizi mahsusi".
Muungano unaoongozwa na Saudia watoa onyo huku wakiandaa oparesheni dhidi ya Houthi mjini Sanaa
Vikosi vya serikali ya Yemen vikipigana na Wahouthi katika mkoa wa Al-Jawf Septemba 15, 2026. / Picha: Maktaba ya AFP.

Muungano unaoongozwa na Saudi Arabia umewataka raia kuondoka katika eneo la kampuni ya mafuta ya Yemen lililoko katika mji wa Sanaa unaodhibitiwa na wapiganaji wa Houthi kwa ajili ya usalama wao huku oparesheni ya mashambulizi ikitarajiwa.

"Kamandi ya Vikosi vya Pamoja vya Muungano huo imeomba raia kuondoka katika eneo la Kampuni ya Mafuta ya Yemen, kituo cha al-Sabaha mjini Sanaa, kwa ajili ya usalama wao," msemaji Turki al-Maliki aliandika kwenye mtandao wa X siku ya Jumanne, akiweka ramani ya eneo hilo lililoko viungani mwa mji.

Awali, muungano huo unaoongozwa na Saudi Arabia unaounga mkono serikali ya Yemen inayotambuliwa kimataifa ulisema hivi karibuni utafanya “mashambulizi mahsusi”.

Msemaji wa muungano huo Turki al-Maliki alisema katika taarifa kwenye mtandao wa X kuwa raia wataagizwa waondoke kwa ajili ya utekelezaji wa “oparesheni mahsusi.”

Mapema, muungano huo unaoongozwa na Saudi Arabia ulisema vikosi vyake vilifanikiwa kuangusha droni tatu kaskazini mwa mji mkuu, Riyadh.

"Tumeziangusha na kuharibu droni 3 kaskazini mwa mji wa Riyadh," msemaji wa muungano huo aliandika kwenye mtandano wa X.

Saudi Arabia imekabiliwa na mashambulizi hatari kwenye viwanja vyake vya ndege na maeneo ya raia katika siku za hivi karibuni huku makabiliano ya kijeshi na wapiganaji wa Kihouthi wa Yemen yakiendelea.

Mapigano kati ya vikosi vya serikali ya Yemen na wapiganaji wa Houthi yameongezeka tangu mapema mwezi Julai kufuatia miezi kadhaa ya hali ya utulivu.

Nchi hiyo imekuwa katika vita tangu wapiganaji wa Houthi wadhibiti mji mkuu Sanaa na mikoa kadhaa kuanzia mwaka 2014, kabla muungano wa nchi za Kiarabu unaoongozwa na Saudi Arabia kuingilia kati mwaka 2015 ukiunga mkono serikali ya Yemen inayotambuliwa kimataifa.