| Swahili
UTURUKI
1 dk kusoma
Erdogan atoa wito wa ushirikiano kati ya nchi za Turkic katika ulinzi, AI na usalama wa mtandao
Migogoro nchini Palestina, Lebanon, Iran, na Ukraine inaonyesha hitaji la "kuimarisha ulinzi wetu na kuongeza ushirikiano wetu katika sekta ya viwanda," Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan amesema.
Erdogan atoa wito wa ushirikiano kati ya nchi za Turkic katika ulinzi, AI na usalama wa mtandao
Erdogan anaunga mkono ushirikiano wa Nchi za Turkic katika ulinzi, AI na usalama wa mtandao wakati wa hotuba yake katika mkutano nchini Kazakhstan / / Anadolu Agency

Rais wa Uturuki, Recep Tayyip Erdogam amesema kuwa migogoro inayoendelea katika eneo hilo imeonesha tena umuhimu wa kimkakati wa nchi za Turkic (mataifa yanayozungumza Kituruki) kufanya kazi kwa mshikamano.

"Migogoro nchini Palestina, Lebanon, Iran, Ukraine, na mingine mingi inaonyesha kwamba tunahitaji kuimarisha ulinzi wetu na kuongeza ushirikiano wetu katika sekta ya viwanda," Erdogan alisema Ijumaa alipokuwa akizungumza katika Mkutano Usio rasmi wa Muungano wa Nchi za Turkic (OTS) huko Turkistan, Kazakhstan.

Erdogan alisema Uturuki inapanga kuimarisha zaidi uratibu na ushirikiano katika usalama wa mtandao wakati wa kipindi chake kijacho cha uongozi, akisisitiza kuwa usalama wa mtandao sasa ni muhimu kama usalama wa ardhini, angani na baharini.

Pia alieleza matumaini yake kuwa nchi za Turkic zitaendelea kuimarisha uhusiano wa kisiasa, kiuchumi na kiutamaduni na Jamhuri ya Kituruki ya Kupro Kaskazini (TRNC).

Akisisitiza ushirikiano wa kitamaduni na kidijitali, alisema alfabeti ya pamoja ya Kituruki inapaswa kutumika kwa upana katika elimu, utamaduni, ushirikiano wa kitaaluma na mabadiliko ya kidijitali.

Aliongeza kuwa mipango ya akili mnemba, ikiwemo mfumo wa lugha ya Kituruki iliyoundwa kuonesha utajiri wa lugha hiyo katika ulimwengu wa kidijitali, inapaswa kuungwa mkono.

CHANZO:Anadolu Agency
Soma zaidi
Amani nchini Ukraine ni muhimu kwa usalama na utulivu wa kikanda: Waziri wa Mambo ya Nje wa Uturuki
Uturuki na India waweke 'tofauti zao kando' na kuangazia agenda chanya: Fidan
Emine Erdogan: Taka Sifuri nguzo muhimu ya hatua ya kuhimili mabadiliko ya tabia nchi
Nini kitarajiwe kutoka kwa ziara ya Waziri wa Mambo ya Nje wa Uturuki Hakan Fidan nchini Bangladesh
Trump kuhudhuria 'mkutano muhimu' wa NATO nchini Uturuki: Rubio
Uturuki, Armenia wafanya mkutano wa biashara Kars kuimarisha uhusiano wa kiuchumi
Spika wa bunge la Uturuki ashtumu UN kutokuwa 'thabiti' katika kuzuia migogoro
Waziri wa mambo ya nje wa Uturuki Hakan Fidan awasili Indonesia ili kuimarisha uhusiano wa kibiashar
Uturuki yatangaza timu ya wachezaji 26 kwa ajili ya Kombe la Dunia la FIFA 2026
Usambazaji wa gesi wa Uturuki, Azerbaijan nchini Syria kutasaidia maendeleo, usalama: Rais Erdogan
Mfumo wa kizazi kijacho wa Uturuki wa BLUEVISION waboresha usalama wa usafiri wa baharini
Erdogan aadhimisha kumbukumbu ya miaka 573 ya ushindi wa Istanbul, anatoa heshima kwa Mehmed II
Uturuki yawakumbuka waliouawa kwenye mashambulizi ya ubaguzi wa rangi ya Solingen 1993
Erdogan aadhimisha Eid al-Adha na ujumbe wa mshikamano wa Gaza, amkemea 'mnyanyasaji' Netanyahu
Erdogan aadhimisha Eid al-Adha kwa ujumbe wa umoja Gaza, amkashifu "muuaji" Netanyahu
Israel inaendelea na uvamizi na mauaji Gaza na Lebanon licha ya makubaliano ya kusitisha mapigano
Uturuki na nchi nyengine 7 zalaani udhalilishaji wa Israel dhidi ya wanaharakati wa Flotilla
Wataalamu wanakusanyika katika Jukwaa la Afrika 2026 ili kujadili uhusiano kati ya Uturuki na Afrika
Idara ya Ujasusi ya Uturuki yanasa washukiwa 10 wa Daesh katika operesheni ya Syria
Uturuki imekuwa kitovu cha nishati, mtetezi wa amani huku kukiwa na mvutano wa kikanda: Rais Erdogan