Iran bado haijatoa maamuzi kuhusu mustakabali wa ushiriki wake katika fainali za Kombe la Dunia mwaka huu, kulingana na chombo cha habari cha nchi hiyo, ISNA.
Katibu Mkuu wa Kamati ya Olimpiki ya Iran alisema kuwa maamuzi ya mwisho yatatolewa na serikali, akiongeza kuwa timu ya taifa ya Iran ipo kwenye mazoezi yake ya mwisho.
Msemaji wa serikali ya Iran Fatemeh Mohajerani alisema kuwa nchi hiyo imejiandaa kwa ajili ya ushiriki kwenye michuano hiyo.
Hapo awali, Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Marco Rubio alikana madai ya Marekani kuweka zuio kwa wachezaji wa Iran kuingia nchini humo, japo alisisitiza kuwa wapo baadhi ya watu ambao hawatoruhusiwa kuingia nchini Marekani.
Akizungumza Aprili 16 mwaka huu, Rais wa FIFA, Gianni Infantino alisema kuwa Iran inatarajiwa kushiriki kwenye michuano hiyo mikubwa duniani.
Michuano ya mwaka huu inaandaliwa kwa pamoja na Marekani, Canada na Mexico na yanategemewa kuanza siku 48 zijazo.














