Licha ya tishio la ugonjwa katika mataifa kadhaa duniani, uzoefu wa taifa la Uganda unatoa mfano wa kipekee wa namna ya kukabiliana na ugonjwa huo hatari.
Taifa hilo lilitangaza kuwa hapakuwa na maambukizi ya Ebola, toka mgonjwa wa mwisho kurusiwa kutoka hospitali ya taifa ya Mulago.
Hatua hiyo ilikuwa ni mwisho wa kampeni maalumu ya afya iliyozaa matunda, ikitokomeza ugonjwa huo toba wala chanjo yoyote.
Uganda ilifikia mafanikio hayo kupitia mbinu thabiti za kubaini na kuchunguza namna ya kuzuia kusambaa kwa ugonjwa huo hatari.
“Ni miezi miwili sasa, na tunafurahi isiyo kifani. Hii inaonesha tunaweza kuishinda ugonjwa wa Ebola kupitia mifumo imara,” anasema Waziri wa Afya wa Uganda, Dkt. Chris Baryomunsi.
Kwa upande wake, Afisa Afya kutoka WHO Afrika, Dkt. Patrick Otim, anaelezea mafanikio kama hatua kubwa katika sekta ya afya ya nchi hiyo.
"Haya ni mafanikio makubwa katika afya ya jamii," anasema, katika mahojiano yake na TRT Afrika.
Uganda ilitangaza mlipuko wa ugonjwa wa Ebola, Mei 15, 2026, na ilipofika Julai 16, 2025, kulikuwa na maambukizi 20 na vifo viwili.
Kati ya maambukizi hayo, matano yalianza nchini Uganda wakati 15 yakitokea nchini DRC.
Ushindi bila chanjo
Tofauti na milipuko ya awali ya Ebola ambapo chanjo ilikuwa sehemu ya kukabiliana na ugonjwa huo, Uganda haikuwa imejitosheleza kwa dawa.
Badala yake, mamlaka za afya nchini humo zilijikita kwenye mbinu mbalimbali kama vile, uchunguzi, kinga na kuwaweka wagonjwa chini ya uangalizi maalumu.
Kulingana na Otim, hiyo ndiyo njia pekee ya kukabiliana kikamilifu na ugonjwa huo.
Wakati wa mlipuko wa ugonjwa huo, kiongozi wa nchi hiyo, Rais Yoweri Museveni aliwaasa wananchi wake kuwa watulivu, akisisitiza kuwa ugonjwa huo huambukizwa kwa njia ya kugusana na sio kwa njia ya hewa.
Aliwataka Waganda kuripoti dalili za maambukizi mapema kwa ajili ya hatua za haraka.
Licha ya nchi hiyo kutokuwa na wagonjwa wowote wa Ebola kwa sasa, ni mapema mno kusema kuwa ugonjwa huo umetokomezwa kabisa.
Shirika la Afya Duniani (WHO) linazitaka nchi kama Uganda kukamilisha siku 42, bila kuripoti mlipuko mwingine.
Katika kipindi hicho, nchi hiyo itakuwa katika uchunguzi hususani wa mipaka ili kubaini kama kuna dalili za maambukizi mengine.
Hata hivyo, mafanikio ya Uganda, yanapaswa kupigiwa mfano na nchi zingine.
"Huu ni ukumbusho kuwa tutilie mkazo suala la kujiandaa mapema," alieleza.
Chanjo mbioni kupatikana
Ingawa Uganda imefanikiwa bila kuwa na chanjo, mlipuko wa Ebola umeongeza kasi ya upatikanaji chanjo kwa ajili ya Bundibugyo.
"Kinachotia moyo ni kwamba watafiti hawatohitaji kuanzia mbali," anasema Otim.
"Tafiti za muda mrefu zinatoa mwanya wa kupatikana msingi wa upatikanaji wa chanjo."
Kati ya taasisi zenye kusukuma ajenda hiyo, ni pamoja na Chuo Kikuu cha Oxford cha nchini Uingereza.
Kwa sasa, changamoto iliyo mbele ya Uganda ni kuongeza wigo wake wa uchunguzi.
Taifa jirani la DRC linaendelea kupambana na ugonjwa huo kwa sasa.
Kulingana na Otim, bado Uganda ipo katika hatari ya kupokea maambukizi kutoka nchi jirani.
Otim anasisitiza umuhimu wa kufanya uchunguzi wa kuvuka mipaka na kutuma timu za wahudumu wa afya wa kutosha.
Uzoefu wa Uganda, unaonesha wazi kuwa hauhitaji chanjo peke yake kukabiliana na ugonjwa kama Ebola.















