Kombora la Urusi laua 3 Mashariki mwa Ukraine

Hata hivyo, Urusi haijatoa tamko lolote kuhusiana na shambulio hilo, licha ya kusisitiza kuwa majeshi yake hayalengi raia wa kawaida.

By
Basi hilo lilikuwa karibu na kijiji cha Nova Oleksandrivka wakati liliposhambuliwa na kombora hilo./Picha:Wengine

Shambulizi lililofanywa na Urusi siku ya ijumaa, limeua watu watatu waliokuwemo ndani ya basi, katika mji wa Kupiansk.

Eneo kubwa la Kharkiv, lililo mpakani mwa na Urusi, lilichukuliwa na majeshi ya Urusi mwezi Februari 2022, kabla ya kuja kukombolewa na Ukraine, miezi michache baadaye.

"Watu watatu waliuawa kufuatia shambulio hilo, dereva wa basi pamoja na abiria wake wawili," walisema wachunguzi wa tukio hilo.

Basi hilo lilikuwa karibu na kijiji cha Nova Oleksandrivka wakati liliposhambuliwa na kombora hilo.

Hata hivyo, Urusi haijatoa tamko lolote kuhusiana na shambulio hilo, licha ya kusisitiza kuwa majeshi yake hayalengi raia wa kawaida.

Mazungumzo ya amani yanayongozwa na Marekani kwa lengo la kumaliza miaka minne ya mapigano kati ya nchi hizo mbili, yameathiriwa na mashambulizi ya Marekani-Israel dhidi ya Iran.