Wapalestina wanavyotumia sanaa kupinga dhuluma na manyanyaso

Kutoka matumizi ya mitandao ya kijamii hadi matumizi ya lugha za picha, Wapalestina wanatumia utamaduni wao kupinga udhalimu na manyanyaso dhidi yao.

By Berire Kanbur
Watengeneza filamu kutoka Palestina.

Vuguvugu la Wapalestina kuhusu kujitawala limedumua kwa muda mrefu na kuchukua mbinu na mielekeo tofauti.

Kwa mfano; vuguvugu la kwanza kabisa lilitegemea ushiriki wa raia, huku la pili likitumia majeshi na vyombo vya habari.

Hata hivyo, leo hii, vuguvugu la tatu linajipambanua kuwa la kiutamaduni zaidi.

Toka kuanzishwa kwa Mamlaka ya Palestina (PLO) mwaka 1964, sanaa imekuwa ni sehemu ya ukombozi wa watu wa Palestina.

Leo hii, utamaduni umekuwa nyenzo muhimu ya utambulisho.

Hivi karibuni, Waziri Mkuu wa Israel alinukuliwa akisema: Tutapambana kwa kutumia silaha zitumikazo uwanja wa vita, hususani zile za mitandaoni.

Kupitia maneno hayo, Netanyahu aliweka wazi ‘Mkakati wa Esther’, propaganda ya Kiisraeli yenye lengo la kuficha ukweli.

Inaripotiwa kuwa, Wizara ya Mambo ya Nje ya Israel, imewalipa watengeneza maudhui Dola 7,000 kwa kila chapisho chanya kuhusu taifa hilo, kwenye mitandao ya TikTok na X.

Lina umuhimu gani hili?

Ukweli ni kwamba, kuonekana kuna nguvu yake.

Nguvu ya simulizi kwenye enzi za kidijiti

Katika kipindi hichi, kilichotawaliwa na maudhui ya kidijiti, kuna nguvu kubwa kwenye sanaa simulizi.

Katika vita hii ya kuonekana, ukweli hushindana na usambazwaji. Wakati serikali zikianzisha kampeni za umma zenye kuhalalisha uvamizi, Wapalestina wameamua kuonesha mateso na manyanyaso yao kupitia sanaa.

Ili sauti zao ziweze kusikika, Wapalestina wameamua kupitisha maudhui yao kwenye majukwaa ya sanaa na utamaduni.

Mitandao ya kijamii, sanaa na fasihi imewaruhusu kujitambua na kuhifadhi historia yao.

Licha za jitihada za Israel kufuta utambulisho wa Palestina kupitia wizi na uharibifu wa urithi wao, Wapalestina wameendelea kuhifadhi tamaduni zao, kuanzia lugha, chakula, mavazi na hata muziki, na kuzigeuza kuwa nyenzo za kujihami.

Mbinu kama Riwaq, ambayo ni ya kihandisi, hutumika kuwaleta Wapalestina pamoja.

Utamaduni si sanaa tu, ni mtindo wa kila siku wa maisha: namna watu wanavyopika,ujenzi, kuimba na kukaa pamoja.

Mwezi uliopita, mchoro wa msanii wa mtaani wa Uingereza Bansky ulidhihirisha hilo.

Katika dunia ya utandawazi ni  muhimu kutumia majukwaa kama haya.

Kuvunja miiko ya utambulisho

Kwa hiyo, utamaduni wa Intifada hauwi ubinifu tu, bali hitaji la kisiasa.

Kwa mfano, linaondoa upendeleo wa wazi kutoka vyombo vya habari vya magharibi na ukandamizaji wa sauti za Wapalestina.

Filamu mbalimbali kama vile Gaza Sunbirds na Holy Redemption zinadhihirisha mwenendo huu mpya.

Kwa mfano, wakati Gaza Sunbirds ikionesha ustahimilivu wakati wa vita huko Gaza, ile ya Holy Redemption inaangazia imani baada ya vita vya Lebanon.

Sanaa hugeuka kuwa lugha mpya wakati lugha yenyewe inapotumika kukiuka haki za wengine.

Berire Kanbur ni mtaalamu wa masuala ya sanaa na utamaduni anayepatikana jijini London na Istanbul.