Rais wa Madagascar Randrianirina amfuta kazi waziri mkuu, baraza la mawaziri
Rais wa Madagascar Michael Randrianirina, ambaye aliingia madarakani kufuatia maandamano ya siku kadhaa Oktoba 2025, amemfuta kazi waziri mkuu na baraza zima la mawaziri.
Rais wa Madagascar Michael Randrianirina, ambaye aliingia madarakani kufuatia maandamano ya siku kadhaa Oktoba 2025, amemfuta kazi waziri mkuu na baraza lote la mawaziri siku ya Jumatatu, msemaji wake alisema katika taarifa.
Randrianirina alichukua uongozi wa taifa hilo la visiwa vya Bahari Hindi kufuatia maandamano yaliyomfanya mtangulizi wake, Andry Rajoelina kuondoka madarakani.
"Hivi karibuni Rais atamteua waziri mkuu mpya, kufuatia utaratibu uliowekwa kulingana na katiba," Harry Laurent Rahajason, mkurugenzi wa mawasiliano katika ofisi ya Rais, alsiema katika taarifa, bila kueleza sababu ya hatua hiyo ya rais.