| Swahili
AFRIKA
1 dk kusoma
Jeshi la Nigeria lasema hakuna ushahidi wa kuuawa kwa raia katika mashambulizi soko la Zamfara
Jeshi linasema mashambulizi ya angani yalizingatia sheria ya kimataifa ya haki za binadamu na kulenga "eneo mahsusi la mkutano" wa viongozi wa wapiganaji.
Jeshi la Nigeria lasema hakuna ushahidi wa kuuawa kwa raia katika mashambulizi soko la Zamfara
PICHA YA MAKTABA: Jeshi limekuwa likishambulia makundi yenye silaha katika jimbo la Zamfara. / Reuters

Siku ya Jumatano jeshi la Nigeria limesema kuwa hakuna ushahidi wa kuuawa kwa raia katika mashambulizi ya angani yaliyolenga wapiganaji jimbo la kaskazini magharibi la Zamfara mwezi huu, kutaja taarifa za idadi kubwa ya watu kuuawa kuwa hazijathibitishwa na za kupotosha.

Shirika la Amnesty International limedai wiki hii kuwa raia wasiopungua 100 waliuawa katika shambulio la angani la Mei 10 kwenye soko lenye watu wengi kijiji cha Tumfa, likitaka mamlaka kuanzisha uchunguzi mara moja.

"Hakuna ushahidi wa kutosha kuwa kuna raia waliuawa katika tathmini yetu rasmi au uthibitisho huru," msemaji wa Makao Makuu ya Jeshi Meja Jenerali Michael Onoja alisema katika taarifa.

Amesema shambulio hilo lilizingatia sheria ya kimataifa ya haki za binadamu na yalilenga "eneo mahsusi la mkutano" wa viongozi wa wapiganaji katika kijiji ambacho walikuwa wamepata taarifa za kijasusi.

Onoja aliongeza kuwa shambulizi kama hilo linakuwa vigumu kuthibitisha kwa haraka idadi ya waliouawa, lakini tathmini baada ya shambulio inaonesha kuwa "magaidi kadhaa walikatwa makali."

Mashambulizi ya jeshi la Nigeria ya angani dhidi ya makundi yenye silaha yamekuwa yakitegemea droni zaidi katika maeneo ambayo makundi yenye silaha yanakuwa misituni na maeneo yasiyofikika kwa urahisi.

CHANZO:TRT Afrika and agencies