| Swahili
UTURUKI
2 dk kusoma
Uturuki yataka Tunisia kumuachia kiongozi wa chama cha Ennahda
Spika wa Bunge la Uturuki, Numan Kurtulmus, amesema Rached Ghannouchi anahitaji matibabu kufuatia umri wake na hali yake ya afya.
Uturuki yataka Tunisia kumuachia kiongozi wa chama cha Ennahda
"Kwa kuzingatia umri wake na matatizo ya kiafya aliyonayo, uzito wa hali ya Ghannouchi haupaswi kupuuzwa," amesema Kurtulmus. / / Anadolu Agency

Spika wa Bunge la Uturuki, Numan Kurtulmus, siku ya Alhamisi ametoa wito kwa kiongozi wa Harakati ya Ennahda na Spika wa zamani wa Bunge la Tunisia, Rached Ghannouchi, ambaye yuko gerezani, kupewa matibabu na kuachiwa kwa kuzingatiwa utu na ubinadamu.

Kurtulmus amesema kupitia NSosyal, mtandao wa kijamii wa Uturuki, kwamba anafuatilia kwa karibu hali ya Ghannouchi, ambaye amemtaja kuwa “miongoni mwa watu mashuhuri katika mapambano ya amani, demokrasia na mshikamano.”

Amongeza kuwa Ghannouchi amesitisha kugoma kula na kutumia dawa, baada ya kuombwa kufanya hivyo na madaktari wanaofuatilia hali yake.

“Kwa kuzingatia umri wake mkubwa na matatizo ya kiafya aliyonayo, uzito wa hali ya Ghannouchi haupaswi kupuuzwa,” alisema Kurtulmus.

Amemtaja Ghannouchi kuwa mtu aliyejitolea maisha yake kwa “mustakabali wa watu wa Tunisia, uhuru, haki na demokrasia,” akisema licha ya shinikizo, na kuishi uhamishoni na kufungwa, hakuachana na “maadili aliyoyaamini na mapambano yake ya kidemokrasia.”

Kurtulmus amesema Ghannouchi amepata kutambuliwa kwa kiwango kikubwa nchini Tunisia na kimataifa kutokana na “msimamo wake wa kidemokrasia wakati wa kipindi cha mpito, msingi wake imara wa kielimu na mawazo yake.”

“Kwa kuakisi uhusiano wa kina wa kindugu uliopo kati ya watu wa Uturuki na Tunisia, namuombea afya njema na natumaini kwamba atarejea katika hali nzuri ya kiafya haraka iwezekanavyo,” alisema.

“Jambo tunalolitamani zaidi ni kwamba apewe kikamilifu msaada wa matibabu unaohitajika, apewe mazingira ya haki na ya kibinadamu yanayohitajika kwa ajili ya kuheshimu utu wa binadamu, na aachiliwe.”

Kuzuiliwa kwa Ghannouchi

Ghannouchi, ambaye alikuwa Spika wa Bunge lililovunjwa na Rais Kais Saied, amekuwa gerezani tangu alipokamatwa Aprili 17, 2023.

Mahakama iliamuru azuiliwe katika kesi iliyohusiana na matamshi yaliyodaiwa kutolewa na yeye, akishtakiwa kwa “kuchochea dhidi ya usalama wa taifa.” Baadaye alihukumiwa kifungo chaa gerezani katika kesi kadhaa, lakini ameyakataa mashtaka hayo na kusema kuwa yana msukumo wa kisiasa.

CHANZO:Anadolu Agency
Soma zaidi
Putin: Uturuki ni mshirika wa kweli wa kiuchumi na wa kidiplomasia
Erdogan, Putin wapongeza ushirikiano wa Uturuki na Urusi katika mkutano wa SCO
Uturuki kuongeza ushirikiano na Muungano wa Ushirikiano wa Shanghai: Rais Erdogan
Mkataba wa Ulinzi wa Makkah waweka msingi wa kujenga mfumo mpya wa usalama wa kikanda: Fidan
Uturuki, Pakistan na Saudi Arabia kufanya mkutano wa kwanza wa makubaliano ya ulinzi ya Makka
Operesheni ya uokoaji inaendelea baada ya kivuko kupinduka karibu na TRNC
Agosti 30: Ushindi uliofungua njia ya kuinuka kwa Uturuki ya kisasa
Erdogan ameisifu Uturuki katika maadhimisho ya miaka 104 ya 'Siku ya Ushindi'
Jeshi la Wanamaji la Uturuki na vikosi vya Somalia vyaokoa meli ya mizigo iliyotekwa na maharamia
Uturuki yataka kupunguza mizozo katika Ulimwengu wa Kiislamu: Erdogan
Rais Erdogan ajadili amani ya kikanda na viongozi wa Rwanda na DRC
Erdogan: Uturuki itaendelea kufanya maendeleo licha ya migogoro ya kikanda
Erdogan na Lula wajadili kuimarisha zaidi uhusiano wa kiuchumi
Katika picha: Waogeleaji 2,500 wavuka Mlango-bahari wa Istanbul katika mbio za kila mwaka za mabara
Uturuki yataka ilani nyekundu ya Interpol dhidi ya Netanyahu kufuatia shambulio dhidi ya fotilla
Uturuki kuimarisha uwezo wa jeshi lake la wanamaji: Waziri wa Ulinzi
Waziri wa zamani wa ulinzi wa Israel Yaalon amshtumu Netanyahu kwa uchokozi dhidi ya Uturuki
Uturuki itaendelea kuwa chanzo cha matumaini kwa Gaza na dunia: Erdogan
Kenya, Uturuki kushirikiana zaidi katika biashara, uwekezaji na ulinzi
Uturuki yachapisha rasmi sheria ya mchakato wa 'Uturuki Isiyo na Ugaidi'