Kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani Papa Leo XIV amewasili nchini Algeria Aprili 13 kwa ziara yake ya kitume.
Hii inakuwa hatua ya kwanza kati ya mataifa ya Cameroon, Angola na Guinea ya Ikweta atakayotembelea wakati wa ziara yake barani Afrika.
Akiwa katika uwanja wa ndege wa Uwanja wa Kimataifa wa"Houari Boumédiène”, Papa Leo XIV alilakiwa na Rais Abdelmadjid Tebboune pamoja na kupewa heshima ya mizinga 21.
Akiwa nchini Algeria, Kiongozi huyo Kanisa Katoliki duniani atapata fursa ya kutembelea mnara wa mashahidi wa Maqam Echahidi, na kutoa salamu zake.
Pia, anatarajiwa kutembelea msikiti mkubwa wa Algiers na baadaye kukutana na jamii ya ndogo ya wakristo katika Kanisa Kuu la Mama Yetu wa Afrika.
Papa Leo XIV anatarajiwa kuzuru mji wa kale wa Annaba, ambao ulikuwa ukijulikana kama Hippo Regius, mahali ambapo Mtakatifu Agustino alihudumu kama Askofu, wakati wa karne ya tano.
Papa Leo XIV anakuwa Papa wa kwanza kuitembelea Algeria, katika historia ya kanisa hilo duniani.










