Je, Umoja wa Afrika unaweza ukapata ufumbuzi kupitia majadiliano Sudan?
AFRIKA
3 dk kusoma
Je, Umoja wa Afrika unaweza ukapata ufumbuzi kupitia majadiliano Sudan?Ziara ya ujumbe kutoka Umoja wa Afrika mjini Khartoum imeashiria mabadiliko kwa serikali ya Sudan kuhusu mpango wa amani wa suluhu ya karibu, lakini utafanikiwa kuleta amani?
PICHA YA MAKTABA: Mwenyekiti wa Baraza la Sudan na mkuu wa majeshi Abdel Fattah al-Burhan wakati akifanya ziara Al Dabbah, Sudan.

Kwa zaidi ya mwezi mmoja, msafara wa mabasi umekuwa ukiwarudisha maelfu ya raia wa Sudan nyumbani kutoka nchi jirani ya Misri walikokuwa wamepata hifadhi kufuatia kuzuka kwa vita vya wenyewe kwa wenyewe 2023.

Wengi wamerudi na kukuta nyumba zao zimeharibiwa, lakini wako tayari kuanzisha tena maisha yao kupitia mpango wa serikali.

Imekuwa miezi saba tangu serikali irudi mji mkuu, Khartoum, kutoka katika mji mkuu wa wakati wa vita, Port Sudan. Mamlaka zimekuwa zikiangazia miradi ya ujenzi upya, inayokadiriwa kugharimu mabilioni ya dola, na kurudisha hali imara ya kisiasa.

Wiki hii, serikali iliulaki ujumbe kutoka Umoja wa Afrika kuhimiza mapendekezo ya majadiliano yanayoongozwa na Wasudan wenyewe kutoka pande zote.

‘Mpatanishi asiyeegemea upande wowote’

“Nafasi ya Umoja wa Afrika inatakiwa kuwa ya mpatanishi asieegemea upande wowote, na kuwaleta pamoja watu wa Sudan kutoka pande mbalimbali na kuratibu upatanishi wa kimataifa na kikanda.”

Kabla ya kuwasili kwa ujumbe wa AU, kiongozi wa nchi Abdel Fattah al-Burhan alishauriana na wanasiasa wa Sudan na makundi ya kiraia kuhusu hatua za kuandaa mazingira kwa ajili ya majadiliano zaidi.

Mapendekezo ni pamoja na kufuta mashtaka ambayo adhabu yake ni kifo kwa viongozi wa upinzani na kuunda kamati ya majadiliano, kulingana na taarifa za vyombo vya habari.

Upatanishi wa karibu

Ziara hii ya ujumbe wa Baraza la Amani na Usalama mjini Khartoum ni ishara ya serikali kukumbatia mpango wa upatanishi wa karibu ambao utajumuisha raia.

Katika mikutano yao kwa nyakati tofauti na Waziri Mkuu Kamil Idris na kiongozi wa nchi Burhan kulikuwa na masuala yanayohusiana na amani, usalama na uthabiti wa Sudan.

Masharti ya majadiliano

Wadau mbalimbali waliozungumza na TRT Afrika walieleza matumaini ya mpango wa majadiliano, licha ya kuwa masuala tata ni kama masharti ya majadiliano yanaweza kukubaliwa na wadau wote nchini Sudan na kukumbatiwa na jamii ya kimataifa. Wengine wametaka mapigano kusitishwa kabisa kabla ya mazungumzo kuanza.

Mariam Al-Mahdi, mwanasiasa wa upinzani na waziri wa zamani wa mambo ya nje, anasema "kuwepo na mazingira salama, yenye uaminifu, na yatakayokuwa na tija". Anasema kuwa hatua ya kuimarisha imani kwa watu siyo suala la kuchelewesha mazungumzo bali kuyalinda majadiliano yasije yakafeli.

Agenda ya mazungumzo

Haijafahamika taarifa za agenda ya majadiliano ziko vipi. Wengi wanaamini kuwa kusitishwa kwa mapigano kutakuwa suala litakalopewa kipaumbele huku mapigano yakiendelea katika majimbo matatu ya eneo la Kordofan na maeneo mengine karibu na mji wa Khartoum.

Kuwepo kwa Umoja wa Afrika katika majadiliano kunaonekana kama ishara ya Afrika kuchukua jukumu la majadiliano na kusisitiza uhuru wa mipaka ya Sudan, huku wakitafuta njia ya kumaliza vita.

Ujumbe wa Umoja wa Afrika mjini Khartoum ulikataa moja kwa moja kuingiliwa na mataifa ya nje katika masuala ya ndani ya Sudan na hatua za njama za kuweka serikali sambamba.

CHANZO:TRT Afrika English