| Swahili
UTURUKI
2 dk kusoma
Vita visivyo na maana Mashariki ya Kati vinaathiri binadamu wote: Erdogan
Erdogan aliangazia athari mbalimbali za kimataifa za mzozo huo, akibainisha kuwa usumbufu unaonekana katika sekta muhimu.
Vita visivyo na maana Mashariki ya Kati vinaathiri binadamu wote: Erdogan
Rais wa Uturuki Erdogan amesema vita hivi visivyo na maana, haramu vinagharimu binadamu wote, sio tu wale wanaohusika. / / AA
tokea masaa 17

Rais Recep Tayyip Erdogan wa Uturuki ameonya kwamba madhara ya vita Mashariki ya Kati yanaongezeka, akisema kwamba athari ya vita hivi inahisiwa na watu wote sio tu pande zinazohusika moja kwa moja.

Akizungumza kwenye Mkutano wa Mikakati ya Nchi wa World Economic Forum Türkiye uliofanyika katika Ofisi ya Dolmabahce sikj ya Ijumaa, Erdogan alielezea vita vinavyoendelea kama “visivyo na maana, haramu, na visivyo vya lazima”, akisisitiza kwamba athari yake inahisiwa na binadamu wote.

“Katika muda wa mwezi mmoja, gharama ya vita hivi visivyo na maana, haramu, na visivyo vya lazima, ambavyo vimeataathiri sana kanda yetu, haijalipwa tu na pande zinazohusika, bali na binadamu wote,” alisema.

Erdogan alibainisha madhara makubwa ya vita kwa dunia nzima, akisema kwamba usumbufu unahisiwa katika sekta muhimu nyingi.

“Madhara hasi ya vita yanahisiwa kote duniani, kutoka kwenye masoko ya nishati hadi utendaji wa uzalishaji, teknolojia ya habari, usafirishaji, na mitandao ya biashara,” alisema.

Alisisitiza kwamba ingawa diplomasia na mazungumzo bado ni njia zinazowezekana za kutatua mgogoro, fursa hizo zinadharauliwa.

“Ingawa kuna nafasi ya kupata suluhu kupitia diplomasia na mazungumzo, sisi, kama binadamu wote, tunabeba mzigo wa kuhujumiwa kwa nafasi hio,” alisema.

Rais wa Uturuki alionya kwamba madhara yatazidi kuwa mabaya iwapo vita vitaendelea.

“Ni ukweli kwamba ikiwa migogoro haitamalizika, gharama itakayolipwa itazidi. Umbali wa kijiografia hautakuwa na maana katika mchakato huu,” aliongeza.

Uturuki imekuwa ikitoa wito mara kwa mara wa kupunguza mvutano katika kanda hiyo huku ikihimiza pande zote kutumis suluhu za kidiplomasia.

CHANZO:AA