Mashambulizi ya kigaidi yaua watu wasiopungua 15 mashariki mwa DRC
Raia wasiopungua 15 wameuawa katika shambulio la kigaidi mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo siku ya Jumatano, kulingana na maafisa wa eneo hilo pamoja na wa mkoa.
Raia wasiopungua 15 wameuawa katika shambulio la kigaidi mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo siku ya Jumatano, kulingana na maafisa wa eneo hilo pamoja na wa mkoa.
Shambulio hilo lilitokea saa moja usiku saa za eneo hilo katika kijiji cha Bafwakoa, kilichoko eneo la Mambasa, Mkoa wa Ituri, maafisa wanasema.
Baptiste Munyapandi, msimamizi wa Mambasa, anasema mamlaka zimethibitisha vifo 15 kufikia sasa, akiongeza kuwa shughuli za kuwatafuta watu zinaendelea na kwamba idadi ya waliouawa huenda ikaongezeka.
Mamlaka zimetaja kundi la Allied Democratic Forces, la kigaidi kuhusika na shambulio hilo mashariki mwa Congo.
Nyumba zimechomwa moto, na watu kutekwa
Nyumba zilichomwa moto, baadhi ya watu waliuawa kwa mapanga na wengine walichomwa moto wakiwa ndani ya nyumba zao, na watu wawili walitekwa nyara, Christian Alimasi, kiongozi wa kijadi wa eneo la Mambasa, alisema.
Mashambulizi ya ADF kwa raia yameongezeka katika miezi ya hivi karibuni katika maeneo ya Ituri na yale ya jirani ya mkoa wa Kivu Kaskazini. DRC na Uganda walianzisha operesheni ya pamoja dhidi ya kundi hilo la kigaidi 2021.