| Swahili
AFRIKA
2 dk kusoma
Vikosi vya Marekani na Nigeria vyawakata makali zaidi ya magaidi 200 kaskazini mashariki
Mashambulizi hayo ya pamoja ya angani yalilenga maficho ya Daesh, ngome zao na miundombinu yao, msemaji amesema.
Vikosi vya Marekani na Nigeria vyawakata makali zaidi ya magaidi 200 kaskazini mashariki
PICHA YA MAKTABA: Kikosi cha Marekani Afrika kinasema kinaimarisha ushirikiano na majeshi ya Afrika yanayopambana na Daesh. / Reuters

Kikosi cha Jeshi cha Marekani barani Afrika (AFRICOM) na wanajeshi wa Nigeria wamewaua magaidi zaidi ya 200 katika operesheni ya pamoja iliyolenga magaidi wa Boko Haram na Daesh kaskazini mashariki mwa Nigeria, pande hizo mbili zilisema siku ya Jumatano.

"AFRICOM, kwa kushirikiana na Nigeria, ilifanya operesheni dhidi ya wapiganaji wa Daesh kaskazini mashariki mwa Nigeria," AFRICOM ilisema katika ujumbe kwenye mtandao wa kijamii wa X. "Operesheni hizi ziliwaangamiza zaidi ya magaidi 200, ikiwemo (kiongozi wa Daesh) Abu-Bilal al-Minuki. Hakuna mwanajeshi wa Marekani au Nigeria aliyedhuriwa."

Msemaji wa Makao Makuu ya Jeshi la Nigeria Samaila Mohammed Uba anasema operesheni hiyo ya pamoja imetatiza sana mitandao ya magaidi katika eneo hilo, huku mashambulizi yakilenga maficho ya wapiganaji hao, ngome zao na miundombinu.

Uba alithibitisha kuwa magaidi zaidi ya 200 waliuawa katika operesheni hiyo na kueleza kuwa ushirikiano huu pia ’ umevipa uwezo na ujuzi wa kijasusi, vikosi vya Nigeria.

Mauaji ya watu wengi

Nigeria imekabiliwa na ugaidi kwa muda mrefu kaskazini mashariki kwa zaidi ya muongo mmoja, hasa kutokana na makundi yenye itikadi kali kama Boko Haram na Daesh. Mapigano hayo yamesababisha vifo vya maelfu ya watu na kuwaondoa mamilioni katika makazi yao, hasa katika majimbo kama ya Borno, Adamawa na Yobe.

Ushirikiano huu unafuatia Marekani na Nigeria kuwa na uhusiano wa kidiplomasia kuhusu vurugu zinazoendelea na unakuja wakati Marekani ikichukua msimamo mkali kwa makundi yenye uhusiano na Daesh barani Afrika.

Mwezi Januari Marekani ilisema kuwa itaongeza silaha zaidi na kusaidia Nigeria na taarifa za kijasusi huku ikiongeza ushirikiano na majeshi ya Afrika yanayolenga kushambulia makundi ya silaha yenye uhusiano na Daesh.

CHANZO:TRT Afrika Swahili