| Swahili
UTURUKI
2 dk kusoma
Erdogan: Tulidhihirisha uhuru wetu baada ya kushinda jaribio la mapinduzi ya 2016
Katika ujumbe wake maalumu wa kukumbuka miaka 10 toka litokee jaribio la mapinduzi la Julai 15, Rais Recep Tayyip Erdogan amesisitiza kuwa Uturuki ilidhihirisha ushindi na umoja wake dhidi ya FETO.
Erdogan: Tulidhihirisha uhuru wetu baada ya kushinda jaribio la mapinduzi ya 2016
Rais Recep Tayyip Erdogan amesisitiza kuwa Uturuki ilidhihirisha ushindi na umoja wake dhidi ya FETO.

Rais Recep Tayyip Erdogan wa Uturuki amelielezea jaribio la mapinduzi la Julai 15, 2016 kama nyakati muhimu katika historia ya Uturuki, akiliita dhihirisho la Uhuru katika miaka 100 ya nchi hiyo.

Katika waraka maalumu wa Julai 15 wenye kichwa cha habari Dhihirisho la Uhuru wa Miaka 100 ya Uturuki, Erdogan alibainisha kuwa jaribio hilo lililofanywa na kikundi cha FETO, halikuwa tu jaribio la kuipindua serikali, bali shambulizi dhidi ya demokrasia na uhuru na utawala wa nchi.

"Usiku wa Julai 15, haukuwa usiku wa jaribio lililoshindikana, lakini ushindi kwa demokrasia, kama ilivyoandikwa ka herufi za dhahabu katika historia, wakati taifa letu lilipolinda uhuru wake kwa gharama za uhai wa watu," aliandika Rais Erdogan.

Watu 253 wauawa, zaidi ya 2000 kujeruhiwa

Kulingana na Erdogan Waturuki walipokea wito wake wa kuingia mitaani kuikomboa nchi yao, ambapo watu 253 na wengine zaidi ya 2000 wakijeruhiwa.

Aliongeza kuwa, utayari huo ulidhihirisha imani kwa “hekima” ya “kidemokrasia”, maono na “ujasiri."

Akirejelea miaka 10 toka lilitokee jaribio hilo, Erdogan amesema kuwa mamlaka za Uturuki zimeendelea na kampeni dhidi ya FETO, ndani na nje ya nchi.

"Tuliitokomeza FETO katika sekta zote, ndani ya serikal, jeshi hata kwenye biashara," alisema Erdogan akisisitiza kuwa mapambano bado yalikuwa yakiendelea.

"Njia pekee ya kukabiliana na FETO na taasisi zenye mrengo kama huo ni kuendeleza kile kilichotokea Julai 15 kwa vizazi vijavyo," aliandika.

Uturuki imeendelea kuwa mshindi ndnai ya muongo mmoja

"Tunaendeleza mapambano yetu dhidi ya FETO na makundi mengine ya kigaidi. Tunapoadhimisha miaka 10, Uturuki inaendelea kuwa yenye nguvu na imara zaidi," alisema.

"Hakuna anayepaswa kuwa na mashaka na mipango ya wadhalimu hawa," aliongeza.

Erdogan alihitimisha kwa kuwakumbuka wale waliojitolea wakati wa jaribio hilo lililoshindwa.

 

 

CHANZO:Anadolu Agency