| Swahili
ULIMWENGU
1 dk kusoma
Guterres: Tunazidiwa nguvu na janga la Mabadiliko ya Tabianchi
Mkutano wa 31 wa Umoja wa Mataifa kuhusu Mabadiliko ya Tabianchi, COP31, unafanyika katika jiji la Antalya, nchini Uturuki.
Guterres: Tunazidiwa nguvu na janga la Mabadiliko ya Tabianchi
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres amewaambia viongozi wanaohudhuria mkutano wa COP31 nchini Uturuki, jitihada zisizoridhisha za kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi, yanazidi kuiangamiza dunia.

Katika hotuba yake, Guterres amewataka viongozi wa dunia kuendeleza mapambano na jitihada za kuikoa dunia kwa ajili ya vizazi vijavyo.

"Tunaelekea kubaya,” alisema Guterres akiangazia ongezeko la uzalishwaji wa hewa ukaa na kupanda kwa viwango vya joto duniani.

Mkutano wa 31 wa Umoja wa Mataifa kuhusu Mabadiliko ya Tabianchi, COP31, unafanyika katika jiji la Antalya, nchini Uturuki.

CHANZO:TRTWorld