Rais Donald Trump wa Marekani amekutana na washauri wake waandamizi wa usalama kuzungumzia pendekezo la ufunguzi wa mlango bahari wa Hormuz.
Wakati huo huo, Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, Marco Rubio amesema kuwa msimamo wa Iran kuhusu njia ya Hormuz, haukufikia matakwa ya Marekani.
ZILIZOPENDEKEZWA
" Hawapaswi kufanya hivyo na hatutowaruhusu kufanya hivyo, kutumia njia hiyo kuamua nani anapaswa kupita na nani haruhusiwi na gharama za kuwalipa ili upite njia hiyo," alisema Rubio.
Hapo awali, Iran iliwasilisha pendekezo jipya kwa Marekanina kutaja kuwa tayari kuachana na udhibiti wake kwenye Mlango-Bahari wa Hormuz ikiwa Marekani itaondoa vizuizi vyake kwenye bandari za Iran, lakini haiko tayari kuujadili mpango wake wa nyuklia.
CHANZO:AFP














