ECOWAS yatangaza hali hatari Afrika Magharibi

Kulingana na Jumuiya hiyo ya Kiuchumi Magharibi mwa Afrika, michakato ya uchaguzi Magharibi mwa Afrika inaendelea kusababisha ukosefu wa amani katika eneo hilo.

By
Tangazo la ECOWAS linakuja siku chache baada ya jaribio la mapinduzi kushindikana nchini Benin./Picha:Wengine / Others

Jumuiya ya Kiuchumi Magharibi mwa Afrika (ECOWAS) imetangaza hali ya hatari, huku eneo hilo likiendelea kukumbwa na hitilafu za kisiasa.

"Matukio ya hivi karibuni yanaonesha mustakabali halisi wa eneo letu katika siku zijazo, na hivyo kuwepo na haja ya kuwekeza kwenye usalama wa eneo letu,” alisema rais wa jumuiya hiyo Oumar Touray katika mkutano wa ngazi ya mawaziri uliofanyika Abuja, nchini Nigeria.

Tangazo la ECOWAS linakuja siku chache baada ya jaribio la mapinduzi kushindikana nchini Benin.

Pia, linakuja wiki chache baada ya mapinduzi ya nchini Guinea-Bissau.

Kulingana na Touray, michakato ya uchaguzi katika eneo hilo ndio kichocheo kikubwa cha kukosekana kwa amani na utulivu katika eneo hilo.