Siku ya Jumanne Afrika Kusini ilipunguza kodi ya mafuta kwa mwezi mmoja ili kuweka bei nafuu ambayo inapanda kutoka na vita vya Iran, huku bei zikiwa juu zaidi ya wakati wowote ule.
Kodi kwa ujumla itapungua kwa randi tatu (dola $0.18) kwa lita moja, mawaziri wa fedha na mafuta walisema katika taarifa ya pamoja.
Licha ya afuweni hiyo, bei ya dizeli itapanda kwa zaidi ya randi 7 kwa lita moja, ikiwa ni ongezeko la asilimia 40%, huku petroli – ambayo bado ni nafuu kuliko dizeli – ikiongezeka kwa asilimia 15%.
Mafuta ya taa, ambayo yanatumiwa zaidi na watu wa kipato cha chini kwa kuwasha taa, joto, na kupika yataongezeka kwa asilimia 93%.
Hatua hii itagharimu serikali dola milioni $352
Hatua hii itagharimu serikali karibu randi dola bilioni sita (dola milioni $352), huku ikitegemea kupata fedha kutoka maeneo mengine, serikali ilisema.
Haikufahamika mara moja namna gani serikali itatathmini upya bajeti yake, huku Waziri wa Fedha Enoch Godongwana akiwaambia waandishi wa habari: "Sijui kwa sasa nitatoa wapi hizi fedha."
Pendekezo la mwaka jana kuongeza kodi ya thamani kwa bidhaa lilisababisha mvutano ndani ya serikali ya muungano ambayo chama cha ANC ilunda baada ya uchaguzi mkuu wa Mei 2024.
"Mikakati inaandaliwa kwa ajili ya hatua za kusaidia watu majumbani na sekta muhimu za uchumi," serikali ilisema.
Vita vya Marekani na Israel dhidi ya Iran
Bei za mafuta zimepanda tangu kuanza kwa vita vya Marekani na Israel dhidi ya kumetatiza meli za mafuta zinazopitia Mlango Bahari wa Hormuz, na kusababisha hali ya taharuki kwa uchumi wa dunia kukiwa na hofu ya uhaba wa mafuta kote ulimwenguni.
Tofauti na nchi zingine katika bara, Afrika Kusinu imeepuka milolongo mirefu ya kutafuta mafuta, ingawa kumekuwa na taarifa za vituo vingine kukosa mafuta huku waendesha magari wakitaka kujaza mafuta.
Mabasi ya abiria, yanayotegemewa zaidi kwa usafiri wa umma, yametishia kuongeza nauli.
















