Mgomo wa wafanyakazi wadumaza safari za ndege katika Uwanja Mkuu wa Jomo Kenyatta, Kenya
Katibu Mkuu wa KAWU Moses Ndiema alisema imepita zaidi ya miaka 11 bila wafanyakazi kupata nyongeza ya mishahara, akiishutumu Mamlaka ya Safari za anga ya Kenya, KCAA kwa kushindwa kushughulikia maslahi ya wafanyakazi.
Mgomo wa wafanyakazi katika uwanja mkuu wa ndege wa Kenya katika mji mkuu Nairobi ulisababisha kucheleweshwa kwa safari za ndege siku ya Jumatatu, Shirika la Ndege la Taifa na waendeshaji wa viwanja vya ndege lilisema.
Shirika la Ndege la Kenya, Kenya Airways lilisema ucheleweshaji katika kitengo cha kudhibiti safari za anga ulikuwa ukiathiri kuruka na kutua kwa baadhi ya ndege katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta.
Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta ni mojawapo ya vituo vikuu vya usafiri wa anga barani humo.
Mgogoro wa wafanyakazi kati ya chama cha wafanyakazi wa anga na mamlaka ya usafiri wa anga kuhusu malalamiko ya wafanyakazi ikiwa ni pamoja na kushindwa kuhitimisha makubaliano ya pamoja ya majadiliano.
Kupitia chama chao cha wafanyakazi KAWU, wahudumu hao walitoa notisi ya siku saba kupatikana suluhisho, la sivyo waanze mgomo wao.
Notisi hii ilitolewa baada ya kusambaratika kwa mazungumzo ya upatanishi yaliyoagizwa na mahakama, ikitaja matakwa muhimu ambayo hayajatatuliwa ikiwa ni pamoja na nyongeza ya mishahara iliyochelewa kwa muda mrefu.
Akizungumza na waandishi wa habari, Katibu Mkuu wa KAWU Moses Ndiema alisema imepita zaidi ya miaka 11 bila wafanyakazi kupata nyongeza ya mishahara, akishutumu Mamlaka ya Safari za anga ya Kenya, KCAA kwa nia mbaya katika kushughulikia maslahi ya wafanyakazi.