Mke wa Rais wa Uturuki, Emine Erdogan amesema kuwa jaribio la mapinduzi la Julai 15, 2016, limedhihirisha ujasiri na watu, huku akiwaenzi wale walioitetea demokrasia.
Kupitia ujumbe wake uliowekwa kwenye mtandao wa kijamii wa Uturuki wa NSosyal, Erdogan alisema Julai 15 ni alama ya mapambano na ujasiri.
"Usiku ule, mashujaa wetu ambao walikuwa ni nuru ndani ya mioyo yao, wamekuwa sauti ya nia yetu, na walinzi wa uhuru wetu," alisema.
Kulingana na Erdogan, ujasiri wa kulinda demokrasia utaendelea kuishi ndani ya kumbukumbu za taifa.
Alisisitiza kuwa, mapambano na sadaka ya kujitoa kulinda demokrasia ya Uturuki, itaishi milele ndani ya taifa.
Alitumia fursa hiyo, kuwakumbuka, na kuwaenzi wale waliopoteza maisha na waliojeruhiwa wakati wa jaribio hilo.
“Kwa shukrani kuu, nawakumbuka mashahidi wa Julai 15,” alisema.




















