Tanzania: Zoezi la kuhama eneo la hifadhi ya Ngorongoro halijafanikiwa

Serikali ya nchi hiyo imekuwa ikihamisha jamii kwenda maeneo yaliyotengwa, kama vile Handeni mkoani Tanga, ili kupunguza mgongano kati ya binadamu na wanyamapori na kuimarisha uhifadhi.

By
Kulingana na Iyombe, kufikia sasa, ni kaya 1,678 pekee zilizoondoka ndani ya NCA, kati ya kaya 23,000./Picha:Wengine

Mwenyekiti wa Tume iliyopewa jukumu la kutathmini utekelezaji wa zoezi la uhamaji wa hiari kwa Wakazi wa eneo la Hifadhi ya Ngorongoro (NCA) kwenda Msomera mkoani Tanga na maeneo mengine, Mussa Iyombe, amesema zoezi hilo halijafanikiwa kama ilivyotarajiwa.

Kulingana na Iyombe, kufikia sasa, ni kaya 1,678 pekee zilizoondoka ndani ya NCA, kati ya kaya 23,000.

“Matokeo ya tathmini yanaonesha kuwa dhamira ya serikali ya kutekeleza zoezi la uhamaji wa hiari ili kuboresha maisha ya wananchi na kulinda ikolojia ya Hifadhi ya Ngorongoro,” alisema Iyombe wakati akikabidhi ripoti ya tume hiyo kwa Rais Samia Suluhu Hassan, Machi 12, 2026.

Alisisitiza kuwa, hadi tume hiyo ikitoka eneo la uwanda wa NCA, kulikuwa na kaya 1,678 ambayo ni ni sawa na asilimia Ngorongoro 7.3 ya kaya 23,000 zinazoishi ndani ya eneo la Hifadhi ya Ngorongoro.

“Kwa takwimu hizi mheshimiwa rais, utaona kwamba zoezi halikufanikiwa kama tulivyokuwa tumetarajia”, aliongeza.

Uhamiaji wa watu kutoka eneo NCA nchini Tanzania, ni mchakato wa hiyari unaoendelea, ukilenga kupunguza msongamano wa watu na mifugo ili kuhifadhi ikolojia na urithi wa dunia.

Serikali ya nchi hiyo imekuwa ikihamisha jamii kwenda maeneo yaliyotengwa, kama vile Handeni mkoani Tanga, ili kupunguza mgongano kati ya binadamu na wanyamapori na kuimarisha uhifadhi.