Rais wa COP31 amezindua muswada wa pili wa maazimio ya Antalya, ambao unaangazia rasilimali fedha, mabadiliko ya tabianchi na ushirikiano wa kimataifa.
Akizungumza wakati wa mkutano wa wanahabari siku ya Alhamisi, Rais wa COP31 Murat Kurum alianisha vipaumbele vitakavayobadili ahadi kuwa uhalisia.
Muswada huo, unaweka msisitizo kwenye lengo la Mkataba wa Paris la kupunguza joto duniani hadi nyuzi joto 1.5.
Kulingana na Kurum, taasisi 167, tayari zimewasilisha michango yao, ambayo pia inajulikana kama NDC.
"Hatua hiyo inatoa ulinzi kwa uhai wetu,” alisema akiangazia athari za kuongezeka kwa nyuzijoto duniani.
Kurum aliongeza kuwa moja ya vipaumbele katika muswada huo ni mkakati wa Uturuki uliopewa jina la 35 kwa 35.
"Kupitia mkakati huu, tunalenga kuongeza mgao wa umeme kwa asilimia 35 ifikapo mwaka 2035," alieleza.
Muswada huo, pia umesisitizia umuhimu wa kupata ufadhili ifikapo mwaka 2035, kwa mujibu wa Kurum.
Kwa upande mwingine, Kurum ametoa wito wa urahisishwaji wa upatikanaji wa fedha na ufadhili katika eneo la Mabadiliko ya Tabianchi.





















