| Swahili
UTURUKI
1 dk kusoma
Uturuki kuwa mwenyeji wa maonesho makubwa ya kimataifa kuhusu ulinzi Istanbul wiki ijayo
Maonesho hayo ya siku sita yanatarajiwa kuleta pamoja sekta ya ulinzi duniani katika maeneo mbalimbali kote jijini.
Uturuki kuwa mwenyeji wa maonesho makubwa ya kimataifa kuhusu ulinzi Istanbul wiki ijayo
Maonesho hayo ya 17 yataoneshwa sanjari katika Kituo cha Maonesho cha Istanbul, Uwanja wa ndege wa Atatürk, Hoteli ya Wow na Atakoy Marina. / AA

Moja ya maonesho makubwa ya masuala ya ulinzi duniani, Maonesho ya Kimataifa ya Ulinzi, yataanza wiki ijayo jijini Istanbul.

Maonesho hayo ya siku sita yataanza Julai 22 na yataandaliwa na Ofisi ya Rais wa Jamhuri ya Uturuki ikishirikiana na Wizara ya Ulinzi ya Uturuki, sekta ya Ulinzi na Wakfu wa Jeshi.

Maonesho hayo ya 17 yatafanyika sanjari katika Kituo cha Maonesho cha Istanbul, Uwanja wa ndege wa Atatürk, Hoteli ya Wow na Atakoy Marina.

Maonesho hayo yataonesha magari ya kivita, magari yenye silaha ya kutumia mbinu vitani, magari ya ardhini yasiyo na dereva, vyombo vya angani, na baharini, mifumo ya silaha, roketi, makombora ya masafa marefu, silaha za kijeshi, michezo ya kijeshi, suluhu za kielektroniki vitani, vifaa vya kuondoa vilipuzi.

Maonesho hayo yanatarajiwa kuhudhuriwa na idadi kubwa ya watu, pamoja na kuwepo kwa hafla kadhaa za kutia saini makubaliano.

Maonesho yaliyopita yalifanyika Julai 2023 jijini Istanbul.

CHANZO:TRT World
Soma zaidi
Watoto hawapaswi kulipa gharama ya vita, ukandamizaji: Erdogan
Uturuki yapiga marufuku mitandao kwa watoto chini ya miaka 15, mabadiliko makubwa ya kidijitali
Hakuna upungufu wa mafuta ya ndege nchini Uturuki: waziri
Wachambuzi wanaonya EU dhidi ya kujitenga na Uturuki huku kukiwa na changamoto za kiusalama
Waziri wa Mambo ya Nje wa Uturuki Fidan kufanya ziara rasmi ya siku mbili nchini Uingereza
Tamasha kubwa la sayansi kwa vijana barani Afrika limefanyika Côte d'Ivoire
Uturuki inakataa ramani za bahari za Ugiriki ikisema kuwa zinakiuka sheria za kimataifa
COP31 huko Antalya kuanzisha enzi mpya ya ushirikiano wa hali ya hewa: Waziri Kurum wa Uturuki
Ishara ya Uganda katika Jukwaa la Diplomasia la Antalya inaonyesha kujitolea kwa uhusiano wa Uturuki
Viwanda vya ujenzi wa meli vya Uturuki katika maonyesho ya US Sea-Air-Space 2026
Uturuki imepongeza uteuzi wa gavana mwenye asili ya Turkmeni katika mkoa wa Kirkuk, Iraq
Erdogan afanya mazungumzo na viongozi wa Burundi, Libya kando ya Jukwaa la Diplomasia la Antalya
Waziri Mkuu wa Pakistan Sharif anaondoka Antalya na sifa kwa Rais Erdogan, kushinikiza uhusiano
Mke wa rais wa Uturuki ahudhuria jopo la 'Moyo Mmoja kwa Palestina' katika Kongamano la Antalya
Rais Erdogan akutana na viongozi wa Slovenia, Comoro, DRC katika Jukwaa la Diplomasia la Antalya
Israel inatumia usalama kama kisingizio cha kunyakua  'ardhi zaidi': Waziri Fidan
Fidan wa Uturuki akutana na mawaziri w mambo ya nje wa Misri, Pakistan na Saudi Arabia
Erdogan aonya kuhusu migogoro ya dunia, ataka diplomasia, utulivu wa kikanda
Viongozi mbalimbali wahudhuria Jukwaa la Kidiplomasia la Antalya
Spika wa Bunge la Uturuki ataka Israel iondolewe Umoja wa Mataifa