Iran yafanya mazoezi ya kijeshi Hormuz kabla ya mazungumzo na Marekani

Mazoezi hayo yanafanyika wakati kukiwa na uhasama mkubwa kati ya nchi hizo mbili.

By
Zoezi hilo, pia linalenga kutathimini mipango ya kijeshi./Picha:Reuters katika eneo hilo la kanda ya Hormuz na kutoa faida ya kisiasa Iran./Picha:

Kikundi cha IRGC nchini Iran kimeanza mazoezi katika eneo la Hormuz, siku moja kabla ya awamu ya mazungumzo na Marekani.

Taarifa iliyotolewa na kitengo cha habari cha IRGC siku ya Jumatatu, kimesema zoezi hilo linalenga kutoa tathimini ya utayari wa vikosi vyake vya majini.

Zoezi hilo, pia linalenga kutathimini mipango ya kijeshi katika eneo hilo la kanda ya Hormuz na kutoa faida ya kisiasa Iran.

Eneo la Hormuz, ni kati ya maeneo muhimu ya kimkakati duniani, likiwa karibu na ghuba na Oman, likiwa pia ni njia ya bahari kutoka ghuba.

Mazoezi hayo yanafanyika wakati kukiwa na uhasama mkubwa kati ya nchi hizo mbili.

Siku ya Ijumaa, Rais Donald Trump alisema kuwa manowari ya pili ya kijeshi ya Marekani itatumwa Mashariki ya Kati.