Maonesho ya Kimataifa ya Ulinzi na Usalama ya Bamako (BAMEX 2026) yamefunguliwa nchini Mali, yakitarajiwa kuonyesha teknolojia mbalimbali za ulinzi na usalama kuanzia tarehe 9 hadi 13 Novemba.
Maonesho hayo yameandaliwa na kampuni ya Uturuki ya ‘The Peak Defence’, chini ya udhamini wa Ofisi ya Rais wa Mali na Wizara ya Ulinzi ya nchi hiyo. Maonesho hayo ya teknolojia za ulinzi yalizinduliwa mwaka jana.
Kampuni za sekta ya ulinzi kutoka Uturuki na nchi nyingine mbalimbali duniani zitashiriki katika maonesho hayo yanayofanyika jijini Bamako.
Aidha, wajumbe kutoka Wizara ya Ulinzi ya Uturuki na Ofisi ya Rais inayosimamia Viwanda vya Ulinzi nchini humo wanatarajiwa kuhudhuria. Vilevile, kutakuwa na wajumbe wa ngazi za juu wa kijeshi na maafisa wa serikali kutoka zaidi ya nchi 40 za Afrika.
Uturuki itawakilishwa na zaidi ya kampuni 20 za sekta ya viwanda vya ulinzi, zikiwemo Baykar, ASELSAN, ROKETSAN, Skydagger na Prontaron Savunma.





















