Mkutano wa 5 wa Elimu uliondaliwa na Taasisi ya Türkiye Maarif waanza jijini Istanbul
Mkutano wa mwaka huu unaangazia matazimio yajayo na mbinu za ubunifu.
Mkutano wa 5 wa Elimu wa Istanbul, ulioandaliwa na Taasisi ya Türkiye Maarif (TMF), umeanza rasmi siku ya Ijumaa.
Mkutano huo unalenga kukuza mijadala kuhusu faida za elimu, kijamii na kiutamaduni duniani.
Tukio hilo, ambalo limefanyika katiku kituo cha utamaduni cha Atatürk, huku kikidhaminiwa na Shirika la Habari la Anadolu (AA), lilifunguliwa na Mke wa rais wa Uturuki, Emine Erdoğan, ambaye pia alikuwa mgeni wa heshima.
Mkutano huo, pia uliwaleta pamoja washiriki wa ngazi za wizara, kutoka mataifa kadhaa barani Afrika.
Katika hotuba yake ya ufunguzi, Rais wa TMF Mahmut Özdil alisema kuwa taasisi hiyo ilizindua mpango mpya wa elimu mwaka 2016 wenye kuonesha uzoefu wa kielimu wa Uturuki kwa washirika wale pamoja na kutoa sauti mpya kwenye nyanja ya elimu.
Kulinga na Özdil, taasisi hiyo inafanya kazi na zaidi ya wanafunzi 70,000 katika mataifa 64 ulimwenguni.
"Toka siku ya kwanza, lengo letu halikuwa kufungua shule pekee," alisema.
"Tunafikiria kuanzisha msingi imara wa kinadharia—ambao utatupa nafasi ya kutafakari falsafa, malengo na mbinu za kielimu, pamoja na kutathmini kazi yetu kikamilifu kama msingi wa kazi yetu."
Aliongeza kuwa, mkutano huo unawapa fursa wadau muhimu kwenye elimu duniani kujadili masuala mtambuka, na kuifanya ndoto ya elimu kuwa endelevu.
Özdil alitumia fursa hiyo kuonesha matabaka kwenye sekta ya elimu, huku akianisha changamoto wanazokumbana nazo watoto walio kwenye mazingira magumu.
Mkutano huo utaendelea siku ya Jumamosi kukiwa na majopo ya mijadala, risala za ufungaji na utoaji wa tuzo.