Rais wa Uturuki aelekea Ethiopia kwa ziara ya kikazi

Erdogan anaelekea Ethiopia ambako atakuwa na majadiliano huku uhusiano wa mataifa hayo mawili, kusainiwa kwa mikataba na mkutano wa pamoja na wanahabari.

By
Erdogan alisindikizwa katika uwanja wa ndege wa Ataturk./Picha:AA

Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan ameelekea nchini Ethiopia kwa ziara ya kikazi.

Erdogan alisindikizwa katika uwanja wa ndege wa Ataturk na Gavana wa Istanbul Davut Gul, Mwenyekiti wa chama cha AK jijini Istanbul Abdullah Ozdemir, na maofisa wengine.

Wakati wa ziara yake, Erdogan atafanya mazungumzo ya ana kwa ana na Waziri Mkuu wa Ethiopia, Abiy Ahmed.

Mbali na vikao hivyo, Erdogan anatarajiwa kuhudhuria hafla ya utiaji saini mikataba mbalimbali pamoja na mkutano wa pamoja na waandishi wa habari.