| Swahili
ULIMWENGU
1 dk kusoma
Melania Trump kuongoza kikao cha Umoja wa Mataifa mashambulizi ya Iran yakiendelea
Kabla ya hapo, Melania Trump amewahi kushiriki kwenye michakato ya kidiplomasia, baada ya kuhusika na kuachiwa huru kwa watoto wa Ukraine, waliokuwa wakishikiliwa mateka nchini Urusi.
Melania Trump kuongoza kikao cha Umoja wa Mataifa mashambulizi ya Iran yakiendelea
Mke wa rais wa Marekani, Melania Trump./Picha:Wengine
tokea masaa 8

Mke wa Rais Donald Trump wa Marekani, Melania Trump anatarajia kuongoza kikao cha Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, kitakachofanyika Jumatatu ya Machi 2, 2026.

Kulingana na taarifa iliyotolewa na ofisi ya mwanamitindo huyo wa zamani, Melania Trump anaingia kwenye vitabu vya historia kwa kuwa mke wa kwanza wa rais aliye madarakani kuongoza kikao hicho.

Hatua hiyo inakuja wakati kukiwa na mashambulizi mfululizo ya Marakeni na Israel dhidi ya Iran.

Kabla ya hapo, Melania Trump amewahi kushiriki kwenye michakato ya kidiplomasia, baada ya kuhusika na kuachiwa huru kwa watoto wa Ukraine, waliokuwa wakishikiliwa mateka nchini Urusi.

Kumeibuka uhasama kati ya Marekani na Umoja wa Mataifa katika miaka ya hivi karibuni, baada ya Marekani kuonekana “ikiingilia majukumu ya umoja huo”.

Wachunguzi wa mambo, wanasema kuwa Rais Trump anajaribu kuingilia wajibu wa Umoja wa Mataifa, kupitia “Bodi ya Amani” aliyoiunda, mwezi uliopita.

CHANZO:AFP