Rais Paul Kagame avielezea vikwazo vya Marekani kama ‘dharau’ kwa nchi yake
Mwezi Machi mwaka huu, Marekani iliiwekea vikwazo jeshi la Rwanda kwa kudaiwa kukiunga mkono kikundi cha waasi wa M23, kinachoendelea kudhibiti eneo la Mashariki mwa DRC, linalodaiwa kuwa na utajiri mkubwa wa madini.
Rais Paul Kagame wa Rwanda amevielezea vikwazo vya Marekani dhidi ya nchi yake kuwa ni dharau na kejeli, akisisitiza kuwa Marekani inaiwekea Rwanda shinikizo kubwa, huku ikionesha upole kwa DRC.
Mwezi Machi mwaka huu, Marekani iliiwekea vikwazo jeshi la Rwanda kwa kudaiwa kukiunga mkono kikundi cha waasi wa M23, kinachoendelea kudhibiti eneo la Mashariki mwa DRC, linalodaiwa kuwa na utajiri mkubwa wa madini.
"Vikwazo hivi havina tofauti na dharau kwa nchi yangu," alisema Kagame katika mahojiano yaliyochapishwa siku ya Ijumaa.
Alisisitiza kuwa, hakuna haja ya Marekani kuonekana “ikitetea upande mmoja”, na “kuupendelea” upande mwingine katika mgogoro huo.
Kulingana na Kagame, Rwanda inaendelea kutimiza masharti yote kwa kuzingatia mkataba uliosainiwa jijini Washington, tofauti na DRC ambayo, alidai kuwa ilikuwa ikitimiza masharti machache tu.